Rais Kikwete kuhutubia katika mkutano wa ILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa viongozi saba duniani ambao watakuwa wageni maalum kwenye Mkutano wa kihistoria wa 100 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) ulioanza Juni Mosi mwaka huu mjini Geneva, Uswisi. Rais Kikwete ambaye ameondoka nchini asubuhi ya leo, Jumanne, Juni 14, 2011, kwa ziara ya siku tatu nchini Uswisi, …

KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA DAVID MSUYA NA MUFTI WA TANZANIA

KATIBU Mkuu wa CCM Wilson Mukama akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, Waziri Mkuu huyo mstaafu alipomtembelea Katibu Mkuu, Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam, jana (LEO). (Picha na Nkoromo Daily Blog) Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba akimkaribisha ofisini kwake, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson …

Mazembe waendelea kupigania rufaa, sasa kutua FIFA

MABINGWA Watetezi wa Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika, TP Mazembe, kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imesema inatarajia kuwasilisha rufaa yake Shirikisho la Mchezo wa Soka Duniani (FIFA), badala ya mahakama ya Upatanishi ya Michezo (CAS). Shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF, iliipiga marufuku TP Mazembe kutetea taji lake baada ya Klabu ya Simba ya Tanzania, kulalamikia …

UFAFANUZI KUHUSU UCHAGUZI WA VILLA SQUAD FOOTBALL CLUB (VILLA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 14 JUNI 2011 1.                   UTANGULIZI.   Hivi karibuni kumekuwa na maelezo mbalimbali katika vyombo vya habari kuhusu uchaguzi wa Klabu ya Villa na wanachama wengine wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). TFF inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusu uchaguzi huo na chaguzi nyingine za wanachama wa TFF.   Kila mwombaji uanachama wa TFF …

WACHAMBUAJI PAMBA WAGOMA KUNUNUA PAMBA!

Na Baltazar Mashaka, TheHabari, MWANZA. BAADHI ya wachambuaji wa pamba mkoani hapa wametishia kugoma kununua pamba  kupinga kukatwa shilingi 100 kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Pamba nchini (CDTF). Wafanyabiashara hao pia wamepinga wakulima kukatwa kiasi kama hicho cha fedha kuchangia mfuko huo kwa madai kwamba, hauwasaidii kikamilifu wakulima wa pamba kupata madawa ya kuulia …

JESHI LA POLISI ARUSHA KATIKA KASHFA!

Na Janeth Mushi, TheHabari, Arusha JESHI la polisi mkoa wa  Arusha limekumbwa na kashfa nzito mara baada ya kuficha majina ya watu watatu waliouawa baada ya kufanya tukio la utekaji na ujambazi kwa wafanyabiashara watano lililojitokeza juzi majira ya saa 7;00 mchana nje kidogo ya mji wa Arusha.