Spika wa Bunge kikaangoni, Chadema wamgeuka

Na Mwandishi wa Thehabari, Dodoma   HATUA ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kumkingia kifua Waziri Mkuu wa Tanzania alipokuwa kujibu baadhi ya maswali bungeni kwenye kipindi cha maswali ya papo hapo kwa waziri mkuu imemponza Spika Makinda. Hali hiyo imekuja baada ya Kambi ya Upinzani Bungeni kuchukua uamuzi    wa kumfikisha Makinda katika Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge …

Wafanyakazi wa Airtel wachangia damu jijini Dar leo!

    Diocles Kaimukilwa, mtaalamu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (kushoto) akichukua damu ya Felix Gama, ambaye ni mmoja kati ya wafanyakazi zaidi ya mia moja wa Airtel waliochangia damu leo hii. Kampuni ya mawasilano ya Airtel hapa nchini imeratibu zoezi la wafanyakazi wake kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa kansa walio katika hospitali …

Timu ya soka Tanzania under 23 yawasili Lagos

Na Boniface Wambura, Lagos Timu ya U23 imewasili salama hapa saa 6.30 mchana kwa ndege ya Kenya Airways kabla ya kuunganisha ndege ya Concord Airlines kwenda Benin City ambapo mechi dhidi ya Nigeria itachezwa kesho kuanzia saa 10 kamili saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 12 kamili jioni. Awali U23 ilikuwa ifike hapa saa 4 kamili asubuhi, lakini …

Press Conference yahairishwa!

    Press Conference iliyopangwa kufanyika leo tarehe 17 Juni, 2011 katika Ofisi za Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imepangwa kufanyika kesho tarehe 18 Juni, 2011 saa 4.00 asubuhi wale wote waliotaarifiwa kuhudhuria Press Conference ya Leo mnaombwa kuhudhuria kesho tarehe 18 Juni, 2011saa 4.00 asubuhi. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Ahsante na kazi njema. Kurugenzi ya Mawasiliano ya …

UTEUZI WA NAIBU GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Daktari Natu El-Maamry Mwamba kuwa Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania. Dkt. Mwamba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt Enos Bukuku, ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi April, 2011. Uteuzi huu unaanza tarehe 13 Juni, 2011. Kabla ya uteuzi huu, Dkt …

Rais Kikwete atolea maelezo tatizo la ajira.

  Upungufu wa ajira hususan miongoni mwa vijana ni changamoto kubwa kwa nchi zinazoendelea kwa sababu ya uchumi wake kuwa mdogo na kukua polepole. Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameyasema hayo Jumatano wiki hii (15 Juni, 2011) wakati akitoa hotuba yake katika kikao cha 100 cha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika makao makuu ya shirika …