Mbunge CCM apewa bendera ya Chadema

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Steven Masele (CCM) amelazimika kupokea bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka kwa vijana wa Kata ya Ndala walioamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwa kile kinachodaiwa wamekosa dira ya muelekeo wa kufanya maendeleo. Akipokea bendera hiyo badala ya kadi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Ndala, jana …

Vijana watolewa Nigeria, Simba waangukia pua Kinshasa

Benin, Nigeria TIMU ya U-23 ya Tanzania imeshindwa kuwatambia vijana wenzao wa Nigeria baada ya kukubali kufungwa mabao 3-0 katika mechi ya marudiano kwenye uwanja wa Samuel Ogbemudia mjini Benin hivyo kutolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania kucheza michezo ya Olimpiki 2012 mjini London. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam vijana wa Tanzania walishinda …

Waziri wa Kenya awapasha viongozi Tanzania

Na Anicetus Mwesa WAZIRI wa Nchi Huduma za Jamii wa Kenya, Dalmas Anyango amewataka viongozi wa umma kutojiona miungu watu, na hivyo kuwatumikia wananchi wanaowaongoza. Amesema watumishi wa umma wanapaswa kutambua kuwa wana deni la kuwatumikia wananchi wao, na kwamba kama kuna mtumishi yeyote hayuko tayari kuwahudumia wananchi kwa kazi ambayo aliiomba ni bora sasa akajiengua mwenyewe katika ofisi aliyoko. …