Rais Kikwete ateta na Dk. Mahathir

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Juni 21, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Tun Dk. Mahathir Mohammad. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye Hoteli iitwayo Prince Hotel and Residence mjini Kuala Lumpur ambako Rais Kikwete amefikia katika ziara yake ya siku nne nchini Malaysia, viongozi hao wawili …

Taswa walaani mwandishi wa Tanzania kudhalilishwa DRC

CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimesikitishwa na kinalaani tukio lililomkumba mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la JamboLeo, Asha Kigundula wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba na DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jumapili iliyopita. Mwandishi huyo pamoja na Watanzania wengine waliokuwa Kinshasa, DRC kushuhudia mchezo wa …

Wanawake wanaotafuta ‘weupe’ kuangamia-TFDA

Na Anicetus Mwesa MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema maelfu ya Watanzania huenda wakaangamia kwa ugonjwa hatari wa Kansa. Imebainishwa kwamba watakaoangamia ni wale wanaotumia vipodozi feki kwa lengo la kutaka kujichubua wawe weupe, ambavyo vina viambata sumu. Hayo yamebainishwa jana na Mkaguzi wa Dawa na Vipodozi wa TFDA, Kissa Mwamwitwa Dar es Salaaam katika Maonesho ya Wiki …

Malecela afanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo

Na Mwandishi wa Thehabari, Dodoma WAZIRI Mkuu mstaafu na mwanasisa maarufu nchini mzee John Malecela amefanyiwa upasuaji wa moyo. Akizungumza mjini hapa jana, Spika wa Bunge Anne Makinda aliwaeleza wabunge Malecela yupo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambapo amefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo na ndio maana hata mkewe, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango …