Wahariri watembelea Hifadhi ya Mikumi Morogoro

WAHARIRI wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, leo wamefanya ziara ya kutembelea Hifadhi ya Mikumi, ikiwa ni moja ya jitihada zinazofanywa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), kuhamasisha utalii wa ndani na kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya habari. Wahariri hao wakiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kigazi, Katibu Mkuu wa Baraza la Habari nchini (MCT), Kajubi …

Mbunge wa CCM amchongea DC Kwa Pinda

Dodoma MBUNGE wa Jimbo la Mvomero mkoani Morogoro , Amosi Makalla (CCM), amemuomba Waziri Mkuu Mizengo Pinda kumchukulia hatua Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwassa, kwa madai amegoma kugawa chakula cha msaada kilihotolewa na Serikali. Makalla amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona Serikali inatoa chakula kwa ajili ya wananchi wake halafu Mkuu wa Wilaya anazuia yasigawiwe kwa wananchi …

Katiba Mpya sasa Aprili 2014 – Pinda

KATIBA mpya ambayo mchakato wake umeanza inatarajiwa iwe imekamilika na kuzinduliwa rasmi Aprili 26, 2014 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema mjini Dodoma leo (Jumamosi Juni 25, 2011). Akifungua Semina Elekezi kwa Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, kwenye ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper, alisema hayo ndiyo …

Mnyika ataka Serikali iwajibike kwa mgawo wa umeme

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema Serikali ina kila sababu ya kuwajibika kutokana na mgawo wa umeme unaoendelea kwani majibu yake juu ya mgawo huo yamekuwa ya kujikanganya yenyewe. Mbunge huyo katika taarifa yake aliyouandikia mtandao huu alieleza kuwa maelezo yanayotolewa na Serikali kuwa mgawo huu umesababishwa na mitambo …