TWIGA STARS KUONDOKA JULAI MOSI KUSHIRIKI COSAFA

TIMU ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka Julai Mosi mwaka huu kwenda Harare, Zimbabwe kushiriki mashindano ya COSAFA yanayoanza Julai 2 mwaka huu jijini humo. Twiga Stars inayofundishwa na Kocha Charles Boniface akisaidiwa na Nasra Mohamed itaondoka saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ikiwa na msafara wa watu 26. Katika …

Mkuu wa Mkoa atoa ambulance Mt. Meru

Mkuu wa Mkoa atoa ambulance Mt. Meru Na Janeth Mushi, Thehabari Arusha OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha imetoa magari mawili yenye thamani ya sh. milioni 253.8 kwa Hospitali ya Mkoa huo ya Mt. Meru kwa ajili ya kubebea wagonjwa. Akikabidhi magari hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidore Shirima alisema lengo la ofisi yake kutoa magari hayo ni …

Hatari, samaki wenye ‘sumu’ Morogoro

Morogoro JESHI la Polisi mkoni hapa limewatahadharisha wakazi wa Manispaa ya Morogoro kutonunua samaki, kwa watu wanaotembeza mitaani kutokana na watu wasiofahamika kumwaga vitu vinavyohisiwa kuwa sumu kwenye Mto Ngerengere. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda wapolisi mkoni hapa Adolphina Chialo alisema watu wasiofahamika walimwaga kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu kwenye mto Ngerengere kwa lengo la kuuwa …

Mkongo wa mawasiliano hauna madhara kiafya-Serikali

Na Lydia Churi-MAELEZO, DODOMA SERIKALI imesema kupitisha mkongo wa taifa wa mawasiliano chini ya nyumba hakuna madhara yoyote kwa afya ya wananchi wanaoishi kwenye nyumba hizo wala kwa nyumba zenyewe. Akijibu swali Bungeni mjini Dodoma leo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga alisema Mkongo wa Taifa hauna madhara yoyote ya kiafya mahali unapopita kwa kuwa hupitishwa chini …

Shibuda aigeuka chadema, aomba posho zibadilishwe jina

Dodoma MBUNGE wa Maswa Magharibi John Shibuda (Chadema) amewaugeuka wabunge wa chama hicho kwa kuitaka Serikali kuongeza posho za wabunge badala ya kuziondoa. Amesema kuwa kwa majukumu ambayo yanafanywa na wabunge hasa wa aina yake ambaye ni mbunge kwa ajili ya maslahi ya jamii na si binafsi ni vema posho zikaendelea kutolewa na kutaka ziitwe malipo ya mwia. Shibuda alitoa …