Marekani yawaumbua Sitta, Mwakyembe yawasafisha Rostam, Lowassa

Na Daniel T. Kamna, Dar es Salaam WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alifanya ziara hapa Tanzania katika shughuli zake mbalimbali nchini alizindua mitambo ya Dowan’s iliyonunuliwa na Marekani na kupewa jina la Symbion. Clinton amesifu mitambo hiyo ya Dowan’s ambayo awali ilibezwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Harrison …

Shibuda , mbowe hapatoshi

MBUNGE wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chadema), sasa ni dhahiri kwamba haafikiani na mikakati ya chama hicho. Wakati viongozi wakuu wa Chadema wakiungana na wabunge wa NCCR-Mageuzi kupinga posho za vikao, Shibuda si tu kwamba anataka ziendelee, bali ziongezwe kutoka Sh 70,000 hadi Sh 500,000 kwa siku. Shibuda alitoa msimamo huo unaokinzana na wa chama chake alipokuwa akichangia makadirio ya …

Mengi atembelea maonesho ya Saba Saba

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akipewa maelezo kabla ya kuanza kutembelea banda kubwa ambalo linashirikisha asasi mbalimbali zinazofadhiliwa na mfuko wa uwezeshaji wanawake unaosimamiwa na Mama Anna Mkapa, katika maonesho ya 35 ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Mpigapicha wa dev.kisakuzi.com).

Ndani ya banda la Airtel viwanja vya Sabasaba

Hapa sio darasani, bali ni ndani ya banda la Airtel katika viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam. Picani ni mmoja wa wahudumu wa Airtel akitoa maelekezo kwa wateja mbalimbali wanaotembelea banda lao kwa kutumia ubao jana.