Ocean View yatolewa Kombe la Kagame

Kikosi cha timu ya Ocean View kilichotolewa Kombe la Kagame. TIMU ya soka ya Ocean View ya Zanzibar, imeaga mashindano ya Kagame Cup baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Etincelle katika mchezo uliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Katika mchezo huo uliamuliwa dakika ya tatu kwa penati ya Nkundwanabake Cadeua baada ya mchezaji Manzi Staley …

Semina ya usajili vitambulisho Zanzibar

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Semina ya wajumbe hao inayohusu usajili wa vitambulisho vya Taifa, iliyoandaliwa na Mamlaka ya Utambuzi na Usajili wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Ukumbi wa Ocean View Hoteli Kilimani Zanzibar Julai 03, 2011. Picha na Ikulu Zanzibar.

Tanzania inapata hasa kwa kutowatambua watu waishio nchini- Dk. Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu Utambuzi wa Usajili na Vitambulisho vya Taifa, katika Ukumbi wa Ocean View Hotel Kilimani Zanzibar leo Julai 03,2011. Picha na Ramadhan Othman, IKULU. Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar JAMHURI ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikipata hasara nyingi kwa …

BAJAJ za wagonjwa zatengenezwa Tanzania

Moja ya bajaj za kubebea wagonjwa ambazo zimenunuliwa nje ya nchi na Serikali. Bajaj kama hizo na zinazosemekana kuwa bora zaidi zinatengenezwa sasa Tanzania. Na Joachim Mushi BAJAJ maalumu za kubebea wagonjwa zenye magurudumu matatu, ambazo Serikali ya Tanzania hivi karibuni imeamua kuzitumia kubebea wagonjwa kutokana na kuwa na gharama ya chini sasa zimeanza kutengenezwa Tanzania. Kampuni ya Comprint International …

Dk. Shein: SMZ imeanza kufanya Mapinduzi ya Kilimo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika uzinduzi wa Uvunaji wa Mpunga wa mbegu, aina ya NERICA, huko katika shamba la kilimo la Mbegu hiyo Bambi Mkoa wa Kusini Unguja jana. (Picha na Ramadhan Othman, IKULU) Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. …

Ndani ya Banda la Wizara ya Nishati na Madini Saba Saba

Kushoto ni baadhi ya wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwaelezea masuala mbalimbali wananchi waliotembelea banda la wizara hiyo Saba Saba jana. Kulia ni baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Nishati na Madini kwenye Maonesho ya Biashara Kimataifa ya Saba Saba yanayoendelea jijini Dar es Salaam wakipewa maelezo anuai katika banda hilo.