Chadema ‘kumshtaki’ Chenge kwa wananchi

Andrew Chenge (MB) Na Mwandishi wa Thehabari, Dodoma MBUNGE wa Singida Mashariki, Tindu Lissu (CHADEMA), amesema Serikali isipomfikisha Mahakamani aliyekuwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge CHADEMA watakwenda mitaani kushtaki kwa wananchi. Amesema kwa mujibu wa sheria za sasa cha Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Chenge anaweza kushtakiwa kwa kuwa ndiye mtuhumiwa namba moja wa kashfa …

Serikali kugharamia utafiti juu ya kinga ya Ukimwi

Na Joachim Mushi RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali ipo tayari kufadhili utafiti wa kinga ya Virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi (VVU), inayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili kwa kushirikiana na wadau kutoka ndani na nje ya nchi. Rais Kikwete alitoa ahadi hiyo kwenye banda la Moi baada ya kupatiwa maelezo ya matokeo ya utafiti wa awali …

JK aofia dawa ya Babu wa Loliondo kutoweka

Na Joachim Mushi RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Idara ya Elimu ya Mimea kuhakikisha mmea aina ya mgarika (sonjo) ambao unatumiwa na Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Ambilikile Mwasapila kutibu magonjwa sugu Loliondo unaifadhiwa ili isitoweke. Rais Kikwete alionesha wasiwasi huo jana alipokuwa akitembelea idara hiyo katika Maonesho ya 35 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja …

Comprint International Ltd ndani ya maonesho ya Saba Saba

Gari la wagonjwa aina ya bajaji lililotengenezwa kisasa likiwa na uwezo mkubwa wa kuhimili miundombinu duni ya barabara maeneo ya vijijini, gari linalotengenezwa nchini Tanzania na baadhi ya vifaa kutoka nje ya nchi lipo katika maonesho ya 35 ya Biashara Kimataifa jijini Dar es Salaam.