Yanga, Simba uso kwa uso fainali ya Kagame leo

Na Joachim Mushi TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam ambao pia ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wanatarajia kupanda uwanjani kupepetana na watani wao wa jadi Simba ya Dar es Salaam. Mchezo huo wa Fainali ya Kombe la Kagame unatarajia kuwa mgumu kwa pande zote kutokana na uhasimu wa soka uliopo kati ya timu zote mbili, ambazo …

TAKUKURU wamnasa Kamanda feki wa TAKUKURU Igunga

Igunga KAMANDA feki wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Stanley Kimaro ametiwa mbaroni na maofisa wa TAKUKURU mjini Igunga baada ya jamaa huyo kujifanya Kamanda wa tasisi hiyo wa wilaya ya Igunga mitaani. Kimaro alikuwa akiwapiga mkwara watumishi mbalimbali wa serikali wakiwemo askari Polisi kuwa yeye ni Ofisa TAKUKURU mgeni wa Wilaya hiyo na kuweza kuwatapeli sh.150,000 …

Mganga anyofoa sehemu za siri za mteja wake na kutoweka

Na Mwandishi Wetu, Urambo MWANAMKE mmoja (66) mkazi wa Kijiji cha Mwendakulima Wilaya ya Urambo mkoani Tabora amefariki dunia baada ya mganga wa kienyeji kumnyofoa sehemu yake ya siri na kisha kukimbia nayo, alipokuwa akipatiwa matibabu kwa mganga huyo. Marehemu huyo, Salome Shikombe jina tunalihifadhi kimaadili ya taaluma hii, alikwenda nyumbani kwa mganga, Kabula Mateo kutibiwa, ambapo hata hivyo haikuweza …

Waziri Sitta amjibu Mbowe

Dodoma WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Kaimu Kiongozi wa shughuli za Bunge, Samuel Sitta amesema, hamshangai Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA) kuiponda Serikali ya CCM na kutaka ilaumiwe kwa kutoimarisha miundombinu vijijini, hali iliyosababisha vijana wengi kukimbilia mijini. Alisema hoja hizo hazina ukweli wowote kwani Serikali ya CCM inajitahidi kwa kila hali …