Yametimia CCM, Rostam ajivua gamba, aachia nafasi zote CCM

Aliyekuwa Mbunge wa Igunga Rostam Azziz. HOTUBA YA MHE.ROSTAM AZIZ KWA WAZEE WA IGUNGA TABORA LEO UTANGULIZI WAZEE wangu, kwanza kabisa kabla ya kueleza kile ambacho kimenisukuma kuzungumza nanyi leo,napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kufikia siku hii ambayo inatukutanisha waja wake. Wazee wangu wa Igunga,baada ya kufanya hivyo napenda pia kutumia fursa hii kuwashukuru ninyi …

Barrick yatoa bilioni 3.2l/- kwa mradi wa maji Shinyanga

KAMPUNI ya uwekezaji kwenye sekta ya madini ya African Barrick Gold (ABG) kupitia mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, itawekeza dola za Marekani zisizopungua milioni 2 (sawa na shilingi 3.2 bilioni) kwenye mradi mkubwa wa maji ambao utawanufaisha maelfu ya wakazi wa eneo hilo. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana jijini Dar es …

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) yadhamini mkutano wa Jukwaa la wahariri Arusha

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania, Absalom Kibanda (wa tatu kushoto) akizungumza na wanahabari leo. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kushirikiana na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), wamendaa mkutano wa kitaaluma wa wahariri utakaofanyika Arusha kuanzia Alhamisi, Julai 14 hadi Jumamosi, Julai 17, 2011. Mkutano huo utawashirikisha wahariri wapatao 80 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambapo mada …

Breaking Newzzzz; Rostam kujivua gamba leo Igunga

MBUNGE wa Igunga, Rostam Azziz leo huenda akatangaza maamuzi magumu kwa kujivua gamba kuendelea na siasa jimboni kwake Igunga mkoani Tabora. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa wadau wake wa karibu ambazo mtandao huu umezinasa mbunge huyo leo anatarajia kujiuzulu masuala ya siasa, jambo ambalo lilikuwa likizaniwa haliwezi kutokea. Taarifa zaidi zinasema Rostam leo amewaita baadhi ya wahariri wakuu …

Twiga Stars yapangwa kundi A all Africa games

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura TIMU ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars) imepangwa kundi B katika Michezo ya Afrika (All Africa Games). Michezo hiyo ya Kumi itafanyika kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu jijini Maputo, Msumbiji. Upangaji makundi kwa ajili ya michezo hiyo kwa upande wa wanawake na wanaume ulifanywa jana na Katibu Mkuu wa Shirikisho …

Wachezaji Eritrea wazamia Tanzania, ni baada ya mechi za KAGAME

WACHEZAJI 13 wa timu ya mpira wa miguu ya Eritrea ya Red Sea mpaka sasa hawajarejea nchini kwao baada ya michuano ya kanda Tanzania, maafisa wamesema. Baada ya Klabu hiyo ya Red Sea kupoteza ushindi wake katika michuano ya CECAFA ya nusu fainali siku ya Jumamosi, ni nusu tu ya wachezaji wote waliingia kwenye ndege kurejea Eritrea. Inaripotiwa kuwa hii …