Dk Chami azungumza na wafanyabiashara wa Japan

Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami akiwa katika mazungumzo na kiongozi wa kundi la wafanyabiashara kutoka Japan waliomtembelea ofisini kwake jijini dsm leo. Wafanyabiashara hao wameonesha nia ya kuwekeza katika maeneo mbali mbali nchini. Kutoka kushoto waliosimama. Balozi wa Japan hapa nchini Bw Hiroshi Nakagawa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami wakiwa katika picha ya …

CCM kujadili tathmini ya kujivua gamba Mbeya kesho

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mbeya kinatarajia kufanya maandamano makubwa, kesho Jumapili Julai 16, yatayofuatiwa na mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya Luanda Nzovwe, jijini Mbeya. Maandamano hayo yatakayoanzia eneo la Mafiati na kuishia viwanja vya Luanda Nzovwe, yatawashirikisha wana-CCM, wapenzi na wananchi wa jiji …

Taarifa mbalimbali muhimu kutoka TFF leo

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura’ STARS KUCHEZA PALESTINA, JORDAN Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) itakuwa na ziara ya mechi mbili nje ya nchi. Stars itacheza mechi ya kwanza Agosti 10 mwaka huu mjini Ramallah, Palestina dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo. Stars ambayo inatarajia kuondoka Agosti 7 mwaka huu kwa ajili …

Wafanyikazi wa BBC waanza mgomo

WAANDISHI habari wengi wanaohudumu katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) wameanza mgomo wa siku moja kulalamikia mpango wa kuwaachisha kazi baadhi yao. Hii inafuatia hatua ya serikali ya Uingereza kupunguza matumizi yake katika sekta ya umma.Wasimamizi wa BBC wamesema hatua ya kuwapunguza wafanyakazi haingeweza kuepukika. Miongoni mwa idara zilizolengwa ni Idhaa ya dunia pamoja na ile inayofuatilia matangazo kote …

Matukio Mkutano wa Wahariri Arusha uliodhaminiwa na SBL

Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Boniface Meena (katikati) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda baada ya awamu ya kwanza ya mkutano wa wahariri wa habari nchini unaoendelea mjini Arusha. Baadhi ya wadau wanaohudhuria mkutano wa wahariri mjini Arusha wakiwa katika mapumziko na kutafakari mada zilizotolewa katika awamu ya asubuhi …

Mbunge Chadema ataka muungano uvunjwe

Dodoma MBUNGE wa Viti Maalumu, Mwanamrisho Abama (CHADEMA), ameiomba Serikali kuridhia Muungano uvunjwe. Abama alitoa kauli hiyo jana wakati akiuliza swali la kwa Waziri Mkuu, Abama alimnukuu Hayati, Abeid Karume ambaye aliufananisha muungano na koti. “Kabla sijauliza swali langu nomba nimnukuu, Hayati Abeid Karume, alisema Muungano wetu ni kama koti, likikubana waweza kulivua mimi naona ni wakati muafaka wa kulivua …