Happy Birthday Mzee Mandela!

Mzee Mandela leo tarehe 18/7/2011, ametimiza miaka 93 ya uhai wake! dev.kisakuzi.com inamtakia afya tele na maisha marefu zaidi mzee wetu huyu.

Rais Kikwete aelekea Afrika ya Kusini kwa ziara ya kidola!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Julai 18, 2011, anaanza Ziara ya kihistoria ya Kidola (State Visit) katika Afrika Kusini, ikiwa ziara ya kwanza ya aina yake kufanywa na Rais wa Tanzania katika nchi hiyo. Rais Kikwete anafanya ziara hiyo kwa mwaliko wa Rais wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Jacob Zuma ambaye utawala wake …

Wabunge nao watembelea maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini Dodoma!

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (CCM) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa mradi wa Biofueli Bi. Ester Mfugale mara alipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini kwenye maonyesho yake yanayoendelea kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma. Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini  Mhe.John Mnyika (CHADEMA) akimsikiliza kwa makini Mtendaji …

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA MTERA!

Mhandisi Mkuu wa Uendeshaji kutoka kituo cha kuzalisha umeme kwenye bwawa la Mtera, Julius Chomolla akitoa maelezo kuhusu kipimo cha kuonyesha maji yamejaa katika eneo hilo. Katika kiuto hicho kiwango cha juu cha kuzalisha umeme ni mita 698 wakati cha chini cha kuzalisha nishati hiyo ni mita 690 na jana (juzi) kipimo hicho kilionyesha mita 690.74, ambapo. Bwawa hilo linazalisha …