Na Deogratius Temba, Iringa
PADRE Salutarius Massawe Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Consolatha aliyefariki amezikwa kwa heshima za kichifu wa kabila la wahehe mkaoni Iringa kwa kupigiwa mizinga 20 angani.
Katika mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Mapadre ya Jimbo la Iringa, yaliyoko Tosamaganga nje kidogo ya Mji wa Iringa, pamoja na maefu ya ndugu, jamaa, marafiki, watawa na wakuu wa Shirika la Consolatha kutoka nchi za afrika marehemu alipewa heshima za kipekee na wananchi wa Iringa huku vilio na zimanzi vikitawala kila kona ya mji huo wakati maiti yake ikipitishwa.
Padre Massawe alifariki Mjini Bagamayo wakati akiogelea katika bahari ya Hindi na wakuu wenzake wa Shirika la Consolatha kutoka nchi mbalimbali waliokuwa na Mkutano katika Kituo cha Kiroho cha Consolatha kilichoko Bunju jijini Dar es Salaam, na baadaye kuhitimisha kwa mapumziko mafupi mjini Bagamoyo. Wakati wa Misa iliyoongozwa na askofu wa Jimbo la Iringa