Oxfam yaja na kampeni mpya ya ‘otesha’

OTESHA ni kampeni mpya ya Oxfam ya juu ya njia bora za kuotesha, kugawana na kuishi pamoja. Ni kampeni yetu sote, mabilioni ya watu tunaokula chakula na zaidi ya wenzetu bilioni moja wanawake na wanaume wanaozalisha chakula hicho. Ni kampeni yenye kutafuta suluhisho kwa mustakabali bora wenye uhakika wa chakula kwa kila binadamu.

Hivi karibuni idadi ya watu itafikia bilioni tisa ulimwenguni na watanzania tutafikia milioni 82 ifikapo mwaka 2050, yaani maradufu ya idadi ya sasa. Ongezo hili la watu ni changamoto kwetu sote na jamii zetu, kwani inabidi  kuotesha/kuzalisha chakula kwa kiwango cha ziada ili kukidhi mahitaji yenye kuongeza kwa kasi. 

Hata hivyo, namna ya uoteshaji an uzalishaji unabidi kubadilika kwa sababu mfumo wa sasa unakaribisha na kuchochoea ukosefu wa usawa na matumizi mabaya ya rasimali tunazozitegemea kama vile ardhi, hali ya hewa na maji. Watu karibu bilioni moja wanalala njaa duniani kote na Tanzania ikiwa moja wapo. Chanzo si upingufu wa chakula duniani bali kukosekana usawa wa fursa na umiliki wa rasimali hizi. Enzi hizi zinatawaliwa na hali mbaya ya hewa, kuongezeka kwa bei za vyakula na kupungua kwa uzalishaji ambavyo vinahatarisha kuwasukuma watu wengi zaidi kwenye baa la njaa.

Uzinduzi wa kampeni ya “OTESHA” ni chachu ya mabadiliko kwani Mfumo uliojikita kwenye maslahi binafsi ya kunafaisha wachache unatuumiza sote wenye mahitaji ya chakula. Ili kukidhi mahitaji ya binadamu wote na kupunguza msukumo hatarishi kwa ulimwengu (sayari yetu), tunalazimika kuotesha katika namna ya usawa na endelevu na kuweka mbele ushirikiano si utengano. 

Watu wachache lakini wenye ushawishi mkubwa, wakiwemo wanasiasa na wafanya biashara wanadai suluhu ni: kilimo cha kisasa (ki-viwanda) ambacho kinashirikisha mashirika makubwa na kutumia rasilimali nyingi zaidi. Na uporaji wa ardhi unaowatumbukiza wanawake na wanaume kwenye lindi la umasikini. Yote haya si suluhisho ni ulaghai kwasababu ni watu wachache tu wananufaika. Kwa upande wa wazalishaji wadogo na masikini nchini, jitihada kama hizo zinapunguza tu dalili na sio kuondoa mizizi ya tatizo.  

Mkakati wa kampeni ya “OTESHA” unahusisha kutafuta suluhisho kwa manufaa ya wengi na si wachache tu. Ili kubainisha hatari zinazotukabili, kuzuia maslahi binafsi na kuongezea nguvu harakati za uoteshaji/uzalishaji kwa mustakabali bora.  Kuleta mabadiliko muhimu kwenye namna au mbinu za uzalishaji, matumizi, na usimamizi wa chakula na rasilimali nyinginezo. Kampeni inahusisha mabadiliko katika maeneo muhimu matatu: uoteshaji, ugawanaji  na namna ya kushi pamoja kwenye ulimwengu.

1. Uoteshaji bora

Tunaweza na inatubidi kuwekeza kwenye kilimo ili kuwawezesha wazalishaji wadogo nchini, ambao ni asilimia 60 wengi wao wakiwa ni wanawake, kuondokana na njaa na kuwapatia rasilimali ili waoteshe zaidi kwa njia endelevu.

2. Ugawanaji wa haki

Tunaweza na inatubidi kubadili usimamizi wa mfumo wa chakula duniani yaani kusimamia masoko ili kuzuia upandishwaji wa bei kiulaghai, kuzuia matumizi mabaya ya uwezo kifedha, uboreshaji wa sera mbaya duniani na katika ngazi ya nchi vilevile kuziwezesha familia na jamii kuhimili mishtuko na mabalaa.

3. Maisha bora

Tunaweza na tunabidi kuanzisha mtazamo mpya yenye mbinu bora za kufanya biashara, kuendesha uchumi wetu and kuishi maisha yetu – mustakabali wenye utajiri wa rasilimali za pamoja, wenye nusura ya hatari za mabadiliko ya hali ya hewa, wenye usawa na wenye kuzingatia yaliyo muhimu kwa maendeleo ya binadamu na vizazi vijavyo.

Jitihada za kufanikisha mabadiliko hayo inafanya GROW kuwa ni kampeni kubwa kuliko zote zilizowahi kufanywa na Oxfam.

Harakati za kufanikisha mustakabali bora zinaendelea kukua duniani. Sisi tunaungana nao. Mkakati ni kushawishi serikali, mashirika makubwa na maarufu na mihadhara mikubwa kama vile Mkutano wa G20. Dhamira ni kuweka baya wale wanaotuangasha na kuwasaidia wanaojenga DIRA mpya na kadhalika kutoa nafasi kwa viongozi wawe jasiri.

Tunashirikiana na wanaharakati wengine ili kuwashirikisha mamilioni zaidi kwenye mjadala kuhusu chakula, maisha bora na mustakabali wa ulimwengu – kuwawezesha watu, kubadilishana ufahamu na kuchukua hatua. Kwa pamoja, tutasukuma serikali zichukue hatua za haraka ili kuzuia mabalaa, kuboresha sera, kuhifadhi rasilimali adimu na kuhakikisha usawa wa haki. Tutasukuma makampuni na kuweka hadharani uporaji wa ardhi unaofanywa na mashirika ya kimataifa na kujinufaisha wao.   Tutashawishi uundwaji wa sera zenye kuwawezesha mamilioni ya wanawawake na wanaume wanaozalisha chakula na mamilioni wanakula chakula hicho. Tutasaidia kujenga mustakabali wenye usalama zaidi, usawa zaidi na matumaini zaidi.       

Mabadiliko yanaanzia kutoka kwa kila mmoja wetu. Kila mara tunaponunua chakula kinachozalishwa katika mazingira ya usawa na endelevu, tunapovuna tulivyovipanda, tunavyosukuma serikali na makampuni kufanya mabadiliko…kwa hakika tunasaidia kuotesha vitu bora.

Kama alivyosema Balozi wetu Steven Kanumba “mfumo wa usawa na endelevu wa chakula unawezekana, kwa pamoja tuondoe ukosefu wa usawa na haki za chakula familia zetu wakati tunapigana tunabadili mfumo wa chakula duniani uwe wa haki kwa wote”

Shiriki kutafuta suluhisho la chakula, maisha na ulimwengu. Ingia kwenye harakati. Tuoteshe njia bora zaidi.