Oxfam wazindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012

Meneja Kampeni wa Oxfam, David Moriarty (kulia), akigawa fomu za kushiriki shindano la ‘Mama Shujaa wa Chakula’ kwa kina mama wa kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo hivi karibuni mara baada ya kuzindua shindano hilo. Shindano la ‘Mama Shujaa wa Chakula’ linaratibiwa na Oxfam kutambuwa na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.

Mkulima na mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula kutoka Nigeria, Briskila Jerome akiwahamasisha akina mama wenzake wa kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo hivi karibuni, kujiunga na shindano la ‘Mama Shujaa wa Chakula’ kwa upande wa Tanzania. Shindano hili linaratibiwa na Oxfam kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.

Wakulima wanawake kutoka vikundi mbalimbali katika kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo wakipata futari baada ya kumalizika kwa mjadala wa hali halisi ya kilimo na uzalishaji wa chakula wilayani humo. Mjadala huu uliratibiwa na Oxfam na kuwahusisha wakulima wanawake kama mpango endelevu wa Oxfam kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.