Ona Manchester United na Man City Wanavyokimbizana Sokoni

nolito_celta

Manchester City imemsajili mshambuliaji wa Uhispania Nolito kutoka kilabu ya Celta Vigo kwa pauni milioni 13.8.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameweka kandarasi ya miaka minne na hivyobasi kuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na klabu hiyo.

Meneja mpya Pep Guardiola tayari amemsajili IIkay Gundogan kutoka Borussia Dortmund kwa pauni milioni 20 pamoja na beki wa Australia Aaron Mooy.

Henrikh Mkhitaryan

Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan amesajiliwa na klabu ya Manchester United ,kulingana na klabu hiyo ya Ujerumani.

Afisa mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema kuwa wamekubali kumuuza mchezaji huyo kwa United ili kumzuia nahodha huyo wa Armenia kuwa ajenti huru mwishoni mwa msimu ujao.

Mkhitayran alijiunga na Dortmund 2013 kutoka klabu ya Ukrain Shakhtar Donetsk kwa pauni milioni 23.