Ofisa wa Sudan Kusini auwawa

KIONGOZI wa wapiganaji wa Sudan Kusini, ambaye alitia saini mkataba wa amani na Serikali, ameuwawa katika hali ya kutatanisha.

Wanachama wa kikundi cha Gatluak Gai wamesema ofisa huyo aliingia katika mtego wa Serikali na kuuwawa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Sudan Kusini imesema aliuliwa na wafuasi wake.

Kanali Gai ni kutoka kabila la Nuer ambalo limekuwa likizozana na Wadinka, kabila kubwa kabisa katika serikali ya Sudan Kusini.

Mwandishi wa BBC alioko Sudan anasema mauaji hayo yatawafanya viongozi wengine wa wapiganaji, kusita kukubali msamaha unaotolewa na rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir.