Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
OFISA ARDHI MANISPAA YA SHINYANGA, ISAICK JOHN AMEFIKISHWA MAHAKAMANI AKIKABILIWA NA MAKOSA YA KUGUSHI PAMOJA NA UTAKATISHAJI WA FEDHA HARAMU HIVI KARIBUNI.
WAKILI WA SERIKALI GEORGE WILIAMU ALIDAI KUWA MTUHUMIWA ALIGUSHI FOMU YA MALIPO NAMBA 00000001 KWENYE PLOT NAMBA 81 BLOCK LL YENYE THAMAN YA SHILINGI MILIONI 99 ILIYOPO LUBAGA MANSPAA YA SHINYANGA KWA JINA LA BLEGANI MAGESE.
WAKILI HUYO ALISEMA KUWA MTUHUMIWA ALITENDA KOSA HILO TAREHE 15, 5, 2012 AKITAMBUA KUWA KUFANYA HIVI NI KOSA AIDHA WAKILI HUYO ALIIYOMBA MAHAKAMA KUTOTOA DHAMANA KWA MTUHUMIWA KWA KOSA LA UTAKATISHAJI WA FEDHA HARAMU KWA KUWA KOSA HILO ALINA DHAMANA.
MTUHUMIWA HUYO ALIKANA MAKOSA YOTE MAWILI MBELE YA HAKIMU MH LIDIA ILUNDA NA KUPELEKWA MAHABUSU HADI TAREHE 11 MWEZI HUU MAHAKAMA ITAKAPOTOA MAAMUZI YA KOSA LA UTAKATISHAJI WA FEDHA KAMA MSHITAKIWA APEWE DHAMANA AU ASIPEWE BAADA YA MAHAKAMA KUJILIZISHA JUU YA PINGAMIZI LA UPANDE WA MASHITAKA.
INADAIWA KUWA HATI HIYO ILIYOGUSHIWA NI MIONGONI MWA HATI ZILIZOMPA DHAMANA MTUHUMIWA WA UFISADI WA FEDHA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU.