Ocean View yatolewa Kombe la Kagame


Kikosi cha timu ya Ocean View kilichotolewa Kombe la Kagame.

TIMU ya soka ya Ocean View ya Zanzibar, imeaga mashindano ya Kagame Cup baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Etincelle katika mchezo uliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Katika mchezo huo uliamuliwa dakika ya tatu kwa penati ya Nkundwanabake Cadeua baada ya mchezaji Manzi Staley kuangishwa eneo la hatari.

Ocean View iliyokuwa ikisubili majariwa kwa Simba ili iweze kuifunga Red Sea kitu ambacho hakikitokea baada kutoka bila ya kufungana. Matokeo ya mchezo wa jioni ambao Simba ingaifunga Red Sea ingeingia moja kwa moja hatua hiyo.

Ocean View imetoka katika mashindano hayo baada ya kuwa na pointi sita w kuwa na wakati Red Sea imekuwa ya pili kwa kuwa na pointi saba, Vital’O imekuwa ya tatu ikiwa na pointi saba na Simba imeongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi nane.

Hatua ya robo fainali Simba itacheza Jumanne na Bunamwaya toka Uganda wakati mchezo wwakati mchezo wa kw kwanza utakuwa kati ya Ulinzi na El Mereikh
Jumatano St. George na Vital’O. na mchezo wa pili utakuwa kati ya Yanga na Red Sea mechi zote zitachezwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo wachezaji wa Simba walionekana kutokuwa makini na kushindwa kumalizia mipira kadhaa wakiwa sentimita chache na goli. Wachezaji wa Simba Ulimboka Mwakingwe, mussa Hassan Mgosi na Said Machaku hawakuwa makini hivyo kushindwa kumalizia mipira wakiwa mita chache na goli.

Wachezaji ambao walionekana kutokuwa makini ni Ulimboka Mwakingwe, Salum Machaku, Rajab Isihaka na Mohamed Banka, wameonekana wamekishindwa kuzitumia nafasi kadhaa walizopata.