Naomba tujikumbushe ahadi za mwana TANU. Just think of their relevance to today’s circumstances. Ignore whether it is Tanganyika,
- Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
- Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.
- Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini , ujinga, magonjwa na dhuluma.
- Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.
- Cheo ni dhamana . Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
- Nitajielimisha kwa Kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote
- Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yangu.
- NItasema kweli daima , fitina Kwangu ni mwiko.
- Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Africa.
- Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa serikali ya Tanganyika.
Ukisoma mwili unasisimka. Nyerere huko aliko lazima anasema ” I TOLD YOU SO”
Dave