SHIRIKA la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), litaendesha kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Tanga. Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Zoezi hili litakaloanzia mkoani Tanga. Linatarajiwa kwenda Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.Zoezi litaanza viwanja vya Tangamano kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.
HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma mbalimbali zitatolewa bure kwenye kambi hizi zikiwemo;
• Upimaji wa Shinikizo la damu
• Upimaji wa sukari kwenye damu – Kisukari
• Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Uzito)
• Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo
• Ushauri nasaha na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
• Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.
Huduma zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE
NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa Tanga kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Wavuvi, Ushirika wa Bodaboda, Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii. Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS, pamoja na Mafao bora mengineyo.
Wananchi wa Tanga wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.
NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.