NSSF Yadhamini Mechi ya Simba na Ndanda FC

Timu zikiingia uwanjani

Timu zikiingia uwanjani

washabiki

Baadhi ya mashabiki wakishhudia mchezo huo.

Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa Mtwara, Bw. Daniel Lyimo akizungumza na waandishi wa habari juu ya shirika la NSSF kuandikisha Wakulima ili waweze kupata mafao ya NSSF yakiwemo, matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi, mikopo ya pembejeo na vifaa vya kilimo, mafao ya kuumia kazini na pension ya uzeeni.

Kikosi cha Ndanda FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme.

Kikosi cha Ndanda FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu, Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu, Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kikosi cha Simba FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme.

Kikosi cha Simba FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme.

21

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupitia mpango wake wa wakulima Scheme imedhamini mechi kati ya Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam na Timu ya Ndanda FC ya Mtwara. Akizungumzia mchezo huo uliofanyika jana mkoani Mtwara, Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume alisema mpango huo umelenga kuwasaidia wakulima mkoani humo.

Alisema kupitia mpango huo NSSF imejikita kuandikisha Wakulima ili waweze kupata mafao yakiwemo, matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi, mikopo ya pembejeo na vifaa vya kilimo. Aliongeza kuwa mpango huo unatoa mafao ya kuumia kazini, pamoja na  pension ya uzeenipindi watakapofikisha umri wa miaka 55.
“..Hii ni kuisaidia serikali kujinasua na mzigo wa kulea wazee kwa kuwaingiza mapema kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF ili waanze kujiwekea kwa maisha yao ya baadae,” alisema Bi. Chiume.

Mpango huo unamwezesha mkulima kupitia chama cha wakulima AMCOS kuweza kupata mkopo na taarifa muhimu kuhusu wakulima,wakulima wanachama wa nssf wanajiunga bure na kuchangia kuazia shilingi 20,000 na kuendelea. Akifafanua zaidi alisema wakulima mbalimbali mkoani Kigoma na wilayani Mbinga tayari wamenufaika kwa kupata mikopo zaidi ya bilioni 3.7 tangu mpango huu wa Wakulima Scheme uanzishwe.

“…Wakulima wote wanakaribishwa kutumia fursa hii kujiunga na NSSF.”

Aidha mpangu huu unampa mkulima nafasi pekee ya kulipa kwa msimu wa mavuno yaani msimu wa mavuno anaweza nlipia kwa mwaka mzima,miezi anayoweza lipa .lakini pia wakulima wanaweza lipia baada miezi iliyopitilizia bila malipo msimu wa mavuno.
NSSF likiwa ni shirika pekee lenye kuwapa huduma ya afya  bure wanachama na kuwawezesha wanachama kutoyumba kiuchumi kwa sababu za gharama za matibabu kwenye familia.

NSSF linawahudumia familia ya mwanachama kwa kuwapa matibabu bure watoto wanne  na mke au mume. Alieleza kuwa matibabu haya wanapata pia wakulima wanaojiandikisha kwenye mpango huu kwa SHIB  ya NSSF na kuwawezesha kuokoa vipato vyao ambavyo vingetumia kwenye matibabu. NSSF mkoa wa mtwara unampango wa kuandikisha wanachama  zaidi ya 63,000 kutoka kwa wakulima wa vijiji na wilaya zote mkoani Mtwara na Lindi  ambazo ni Tandahimba, Nanyumbu, Masasi, Nachingwea, Newala, Mtwara Vijijini ambao wengi ni wakulima wa  zao korosho.

aidha wakuliwa wataweza kupata mikopo kupitia SACCOS zao na kuwawezesha kununua mbolea,madawa ya kuulia wadudu, pembejeo, zana mbali mbali za kilimo ili kujiinua kiuchumi kupitia NSSF SACCOS Loans, Ofisi ya NSSF Mkoa wa mtwara umeshatoa jumla ya shilingi Bilion  1.75 kwa SACCOS zilizokidhi vigezo na kuwainua kimaisha wajasilia mali, wakulima na wafanyakazikwenye mkoa huo. Mpango huu wa Wakulima Scheme ulizinduliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete Mwezi Mei mwaka huu.

Mr Dalali akitoa shukran kwa waandalizi wa ndanda day na wadhamin wa mpambano ambao ni NSSF kwa kuwezesha timu hizo kupambana kwenye mechi ya kirafiki baina ya timu hizo.Kwa mara ya mwisho timu ya mtwara kucheza mpira ilikuwa ni miaka kumi iliyopita

Bw. Dalali akitoa shukran kwa waandalizi wa ndanda day na wadhamin wa mpambano ambao ni NSSF kwa kuwezesha timu hizo kupambana kwenye mechi ya kirafiki baina ya timu hizo.Kwa mara ya mwisho timu ya Mtwara kucheza mpira ilikuwa ni miaka kumi iliyopita