NPP Mahakamani Kupinga Matokeo Ghana

CHAMA Kuu cha Upinzani nchini Ghana kimewasilisha kesi katika mahakama kuu zaidi nchini humo kupinga ushindi wa rais John Mahama katika uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi huu.

Chama cha National Patriotic Party (NPP) kimepinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika tarehe Saba Desemba, ikidai ulikumba na udanganyifu mkubwa.

Tume ya uchaguzi nchini humo ilisema kuwa Bwana Mahakama alipata asilimia 50.7 ya kura zote zilizopigwa, idadi ambayo ni kubwa na hivyo kuepuka duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya mgombea wa chama cha NPP Nana Akufo-Addo, ambaye alipata asilimia 47.7 ya kura.

Waangalizi wa kimataifa walisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

Chama hicho cha NPP, kimesema imewasilisha kesi hiyo baada ya kuchunguza takwimu kutoka kwa vituo elfu ishirini na sita vya kupigia kura, vilivyokujwa na zaidi ya kura milioni kumi na moja.

Akufo-Addo alishindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais mwaka wa 2008, kwa asilimia moja lakini alikubali matokeo hayo.

Bwna Mahama wa chama cha National Democratic Congress party, alikuwa makamu wa rais wa Ghana hadi kifo cha ghafla cha rais wa hiyo hiyo John Atta Mills, mwezi Julai mwaka huu, ambako aliteuliwa kuhudumu kama kaimu rais wa nchi hiyo.

Taifa la Ghana limekisiwa kuwa nchi iliyo na demokrasia iliyokomaa na thabiti zaidi barani Afrika.

-BBC