NMB yawezesha kufanyika kwa mashindano ya michezo Zanzibar

Makamu wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru Kaimu Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya NMB, Abdulmagid Nsekela kwa niba ya NMB kwa udhamini walioutoa ili kufanikisha mashindano hayo.

 

Makamu wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru Kaimu Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya NMB, Abdulmagid Nsekela kwa niba ya NMB kwa udhamini walioutoa ili kufanikisha mashindano hayo.

 

Kaimu Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wakati NMB Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano ya michezo ya taasisi za Elimu ya juu na Vyuo vikuu mjini Zanzibar.Uzinduzi huu ulifanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Amani na kuhudhuliwa na wageni mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais Mhe. Balozi Idd. NMB na Sanlam kampuni ya Bima nchini wakiwa ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo.

 

Mkuu wa Mkoa mjini Zanzibar Mhe. Ayoub Mohamed (Pili Kushoto) akiwa kwenye kikao cha kuwashukuru wadhami wakuu wa mashindano hayo ya Michezo ya taasisi za elimu ya juu pamoja na vyuo vikuu mjini Zanzibar. Kikao hiki kilifanyika mara baada ya uzinduzi rasmi.

 

MAKAMU wa Rais wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd, ameipongeza Benki ya NMB kwa kudhamimi Mashindano ya Michezo kwa Taasisi za Elimu na Vyuo Vikuu Zanzibar (ZAHILFE 2017), iliyozinduliwa juzi Jumapili, huku akiwataka washiriki kuitumia vema fursa hiyo. NMB imedhamini mashindano hayo kwa kiasi cha Sh. Mil. 20, ambako timu kutoka taasisi za elimu na vyuo vikuu Zanzibar, vitachuana hadi Mei 26, bingwa wa mashindano hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, atakapopatikana.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo, Balozi Idd, aliishukuru NMB kwa kuipa umuhimu mkubwa na kudhamini mashindano hayo, huku akichagiza washiriki kuonyesha vipaji, ili kujijengea wigo wa mafanikio michezoni.

“Tunawashukuru na kuwapongeza wafadhili wa mashindano haya, Benki ya NMB pamoja pamoja Sunlam, kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na vijana wetu hapa Zanzibar. Ombi langu kwa vijana, ni kuitumia fursa hii kujinufaisha kimichezo, kwani michezo ni ajira kwa sasa,” alisema Balozi Idd.

Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Abdulmajid Nsekela, aliushukuru uongozi wa ZAHILFE kwa kuona umuhimu wa kuifuata NMB kuomba udhamini, akisema beki hiyo ni mahala sahihi pa kukimbilia katika michezo.

“Tulipopata maombi ya kushiriki mashindano haya, tulifurahi sana kwani hii ilionyesha ni jinsi gani mmetambua umuhimu wa NMB katika michezo.

“Tunajivunia kuwa nanyi katika wiki hii nzima na pia tunaomba wanafunzi pamoja na wazazi watembelea banda la NMB, lilipo viwanjani hapa ili wapate Elimu ya Huduma za Kibenki.” alisema Nsekela.

Zaidi ya wanafunzi 2,000 kutoka Taasisi za Elimu na Vyuo Vikuu Zanzibar, wanatarajia kuchuana katika michezo mbalimbali ikiwemo soka, netiboli, kikapu, mpira wa meza (table tennis) na mingineyo, kusaka mabingwa wa ZAHILFE 2017.