NMB YASHINDA TUZO YA BENKI BORA YA MAENDELEO AFRIKA 2017

Makao Makuu ya Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.

 

BENKI ya NMB PLC imeshinda tuzo mbili katika sherehe za utoaji wa tuzo wa benki bora duniani zilizofanyika Jijini London, Uingereza. NMB Imetajwa kwa mara ya kwanza kuwa ni Benki Bora ya Maendeleo Barani Afrika huku tuzo ya pili ikiwa ni Benki Bora Tanzania 2017 hii ni mara ya Tano Mfululizo.

Kila Mwaka, Jarida la Euromoney huandaa hafla ya kuyatambua zaidi ya Makundi 20 ya bidhaa za kitaasisi za kifedha zikiwemo benki kote duniani kwa kuagalia benki bora na ya kiwango cha juu kwa kila bara na benki bora katika nchi takribani 100 duniani kote. Tuzo hii huzitambua taasisi za kifedha duniani kote ambazo zimepata mafanikio ya hali ya juu katika maeneo yao, kwa kuonyesha ugunduzi na kupata mafanikio ya kifedha kila mwaka.

Jarida ya Euromoney liliandika kuwa,“NMB siyo benki iliyo hai bali ni benki inayofanya kazi. Maamuzi makubwa yanafanyika kwenye maeneo ya mtaji, biashara na watu yamekuwa yanafanyika. Katika maboresho hayo, bado benki imeweza kutoa gawio zuri kwa wanahisa kuliko taasisi yoyote ya fedha nchini.”

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema kuwa ubunifu katika huduma, tekinolojia na uwekezaji katika fedha za kielektroniki kwa msaada wa mtandao mpana wa matawi na ATM imechangia kuiboresha benki na kuifanya taasisi bora ya kifedha nchini.

“Kutatua changamoto za jamii ya watu wasiotumia huduma za kibenki nchini inachukua uwekezaji, ubunifu na uwezo wa kuwaleta wadau katika malipo na huduma zingine za kifedha,” alisema Bi. Ineke

Bi. Ineke alisema “kuwa ushindi wa tuzo mbili kwa mpigo za benki ya maendeleo Afrika na benki Bora Tanzania ni kielelezo tosha kuwa juhudi zetu zinaonekana situ Tanzania bali Afrika nzima.”

“Tunatoa shukrani zetu wa wateja, wafanyakazi na washika dau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya makubwa kwa benk, “alisema Bi Ineke na kuongeza kuwa NMB itaendelea na ahadi yake ya kuwapa huduma bora wateja wake sasa na siku za mbeleni.

Akizungumza kwenye hafla, Mhariri wa jarida la euromoney Bwana Clive Horwood alisema “mchuano wa kupata tuzo mwaka huu ulikuwa wa ushindani sana katika taasisi zilizoshiriki na hivyo kufanya uamuzi kuwa mgumu sana Benki zilizoshinda na kujipatia tuzo zetu zimechukua hatua kubwa katika mipango yao ya kibenki. Mabenki huko miaka ya mbele yatakuwa yanaangalia nini unafanya na pia nini ambacho hukifanyi. Mwaka huu, benki zilizong’ara zimetafsiri kwa unaga ubaga ni wapi kwenye nguvu Zaidi na kuzingatia maeneo hayo.”