Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akimkabidhi baba wa watoto pacha wanee, Abednego Andrew Mafuluka mkazi wa Kimara Mwisho, Dar es Salaam mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni msaada kwa mapacha hao wanne. Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi cha shilingi milioni 10, kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye. Wa pili kulia ni mama mzazi wa mapacha hao, Sara Dimosso akiwa kabeba watoto wake huku akisaidiwa na nduguye.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akimkabidhi mama mzazi wa watoto wanne mapacha, Sara Dimosso (kulia) mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni msaada kwa watoto mapacha wanne aliojifungua hivi karibuni. Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi milioni 10 ikiwa ni kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye. Katikati ni baba wa watoto pacha wanee, Abednego Andrew Mafuluka akishiriki kupokea msaada huo.
Mama mzazi wa watoto mapacha wanne, Sara Dimosso (kulia) pamoja na mume wake, Abednego Andrew Mafuluka (katikati) wakipiga picha ya pamoja na mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 iliyokabidhiwa na Benki ya NMB ikiwa ni msaada kwa watoto mapacha wanne aliojifungua hivi karibuni. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi mara baada ya kuwakabidhi, Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi milioni 10 ikiwa ni kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika picha na familia ya Bwana na Bibi Abednego Andrew Mafuluka pamoja na watoto wao mapacha wanne mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya msaada.
Bwana Abednego Andrew Mafuluka (katikati) akizungumza kuishukuru Benki ya NMB baada ya kuguswa na kuamua kuwasaidia watoto wao mapacha wanne.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akizungumza kuelezea namna Benki ya NMB ilivyoguswa na kuamua kuwasaidia watoto hao mapacha wanne waliozaliwa pamoja.
BENKI ya NMB imetoa kiasi cha shilingi milioni 10 ikiwa ni kuwasaidia watoto mapacha wanne waliozaliwa na familia ya Bwana Abednego Andrew Mafuluka mkazi wa Kimara Mwisho, jijini Dar es Salaam. Familia hiyo iliamua kuomba msaada baada ya Bi. Sara Dimosso mke wa Andrew Mafuluka kujifungua mapacha wanne ambao wameelemewa kimalezi huku wakiwa na kipato cha kawaida.
Akikabidhi msaada huo Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi nyumbani kwa familia hiyo Kimara Mwisho alisema NMB imeguswa na kilio cha familia hicho kuomba kusaidiwa kimalezi kutokana na kuzidiwa hivyo wameamu kutoa shilingi milioni kumi ambazo zimeingizwa katika akaunti za watoto hao ili ziweze kuwasaidia wazazi na watoto hao hata hapo baadae.
“Kwanza tunawapa hongera sana sisi kama NMB tumeguswa na tukio hili kwani ni tukio ambalo linatokea mara chache sana katika jamii, kwa kuwa NMB iko karibu sana na jamii tunatwapa kiasi cha shilingi milioni 10, kiasi hicho tumewapa kama kuwekeza kwa watoto katika malezi na mahitaji mengine ambayo ni muhimu yanayoitajika. Pia tunaishauri jamii iwe karibu na benki yetu kwani ni benki ambayo inagusa jamii moja kwa moja,” alisema Evelyne Mushi.
Aidha Meneja huyo wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, aliongeza kuwa wamewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea fedha hizo shilingi milioni 10 ikiwa ni kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye.
Kwa upande wake Bwana Abednego Andrew Mafuluka aliishukuru Benki ya NMB kwa kujitokeza kuwasaidia ili aweze kukabiliana na changamoto za malezi ya mapacha hao wanne pamoja na watoto wengine wawili wa mwanzo. Aliwaomba watu wengine wenye kuguswa kumsaidia chochote ili waweze kuwahudumia mapacha hao. Kipato cha familia hiyo ni cha kawaida na wamekuwa na changamoto ya malezi tangu wajaliwe mapacha hao.
Mama mzazi wa watoto mapacha wanne, Sara Dimosso (kulia) pamoja na mume wake, Abednego Andrew Mafuluka akizungumza kuishukuru Benki ya NMB kwa kuwasaidia shilingi milioni 10 iwawezeshe katika malezi ya watoto hao.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika picha na familia ya Bwana na Bibi Abednego Andrew Mafuluka pamoja na watoto wao mapacha wanne mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya msaada.