NMB, Mgahawa wa VVK wafanikisha futuru ya watoto yatima zaidi 450 Dar

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Banki ya NMB, Omary Mtiga akizungumza na zaidi ya watoto 450 waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam. NMB kwa kushirikiana na Mbunifu wa Mavazi nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau wengine katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika wamefanikiwa kufuturisha watoto hao yatima kutoka vituo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam.

 

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Banki ya NMB, Omary Mtiga (wa pili kulia) akitoa zawadi kwa watoto walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na Mbunifu wa Mavazi nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau wengine ikiwemo Benki ya NMB katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Shabaan Robert uliopo Upanga na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali pamoja na wadau waliosaidia kufanikisha jambo hilo wakiwemo NMB na wengine.

 

Baadhi ya watoto waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam wakiwa katika futari iliyoandaliwa na NMB kwa kushirikiana na Mbunifu wa Mavazi nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau wengine katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

 

Sehemu ya watoto waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam, wakiwa katika futari iliyoandaliwa na NMB (mdhamini) kwa kushirikiana na Mbunifu wa Mavazi nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau wengine katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika..

 

Sehemu ya zaidi ya watoto 450 waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam wakiwa katika futari hiyo kwenye Ukumbi wa Shaan Robert.

 

Sehemu ya zaidi ya watoto 450 waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam wakiwa katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwenye Ukumbi wa Shaan Robert.