BENKI ya NMB kwa kupitia tawi lake la NMB Zanzibar imeandaa hafla na kuwakusanya wateja wake wadogo na wakati ambao ni wanachama wa klabu ya biashara ijulikanayo kama “NMB Business Club” ili waweze kuzungumza nao katika ufanikishaji wa biashara zao lakini pia kutoa mafunzo ya kibishara.
Hafla hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi na Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar, Khatibu Abdulrahman Khatibu ilifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wafanyibiashara zaidi ya 200 wa mjini Unguja. Kusudi kubwa la hafla hii ni kutaka kusikia kutoka kwa wafanyabiashara wa mjini Zanzibar mahitaji waliyokuwa nayo lakini pia kuwapa semina elekezi ili kufikia malengo ya bishara zao.
Ingawa Benki ya NMB imekua na utamaduni wa kukutatana na wateja wake wa Nyanja tofauti tofauti katika nyakati tofauti ili kuwaelezea maendeleo na huduma mbalimbali ambazo NMB inakua imezifikia kwa kusudi la kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja wake.
Sisi kama NMB tunayofuraha kubwa sana na tunajivunia kuwa na wateja wetu leo na tunaamini kwa kupitia mkutano huu na mafunzo ambayo leo mmeyapata yatakuwa mwongozo kila mnapofikiria kukua kibishara zaidi sana nawasihii mzingatie yale yote yaliyotolewa na watoa maada lakini zaidi mzingatie wosia wa mgeni rasmi Mheshimiwa Khatibu.
Naamini mkiwa na nidhamu katika matumizi ya fedha hasa mikopo ambayo mnayohukua mtafika mbali kibiashara. Alisema Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam” – Vicky Bishubo.
Naye mgeni rasmi katika hafla hii Mhe. Khatibu Abdulrahman Khatibu aliwasihi sana wafanya biashara hao kua na nidhamu ya Mikopo inayochukuliwa. Alisema wengi wa wafanya biashara hupotoka mara wanapopata mitaji ya bishara zao hudhani kua pesa itabakia katika mikono yao siku zote. Aidha aliupongeza uongozi wa benki ya NMB kwa kuona haja ya kuwa na klabu ya biashara ambayo kusudi lake ni kuwa karibu na wateja wao ili kuhakikisha wanafikia malengo ya biashara zao.
“Kwanza kabisa ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa benki ya NMB nkwa kuona umuhimu wa kuwa na klabu ya biashara hapa Mjini Unguja. Klabu hiii iwe chachu ya maendeleo kwenu wafanyabishara wa Zanzibar ili kusudi hata wale ambao wamekua waoga wa mikopo na waoga wa kufanya biashara wapate ujasiri kutoka kwenu.
Lakini pia nitoe angalizo kwenu wafanya biashara, Msibweteke na pesa mnazozipata msidhani pesa hizo zitakaa mikononi mwenu siku zote. Mnatakiwa kuwa na nidham katika matumizi yenu ya Pesa Mafunzo mnayopewa yakawafae ili muweze kufikia malengo ya Biashara zenu”. Alisema Mhe. Khatibu Abdulrahman Khatibu.
Benki ya NMB imfanikiwa kuzindua klabu za bishara (Business Clubs) katika mikoa yote nchini. Ili kuhakikisha kuwa wanakua karibu na wateja wake NMB imekua ikifanya mikutano na wanachama wa klabu hizi kila mwaka ili kusikia changamoto amabazo wanakutana nazo.
Lakini pia kuwaelezea wateja wao uboreshwaji wa huduma mbali mbali za kibenki ambao NMB umefanya.NMB wanatoa wito kwa wateja wao kutokua waoga wa kufanya biashara na kuchukua mikopo Benki. “Benki ndiye rafiki wa karibu wa mfanya biashara yeyote, ‘NMB wanasema Mvute mmoja tukue pamoja’.