
Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mhandisi Dk. Crispin Kinabo akiwasilisha mada juu ya utunzaji wa mazingira kwenye migodi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika mapema leo katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Mafunzo hayo yalishirikisha viongozi na watendaji wa wilaya, madiwani, wakuu wa vitongoji na wachimbaji wadogo lengo lake likiwa ni kuwapa uelewa wa kanuni za uchimbaji bora wa madini.

Mmoja wa wakilishi wa wachimbaji wadogo ambaye ni mmiliki wa mgodi katika eneo la Mhesi Mapinduzi lililopo wilayani Tunduru Bi Sofia Hamdan akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.