Hapa mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
WIZARA ya Nishati na Madini imetangaza nafasi za masomo kwa vijana wa Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China kwa kipindi cha mwaka 2015.
Hayo yalibainishwa na Msemaji wa Wizara hiyo Badra Masoud Dar es Salaam leo wakati akizungumza na wanahabari.
Alisema nafasi hizo za masomo ni ngazi ya Shahada ya Juu ya Uzamili katika fani ya gesi katika Chuo Kikuu cha Jiosayansi cha China ambapo muda wa kutuma maombi hayo umeongezewa hadi kufikia Machi 30 mwaka huu.
Alisema waombaji wa ufadhili huo wanatakiwa kuwa na Shahada ya Sayansi ya Ardhi au Uhandisi kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali, na muombaji awe na miaka kati ya 35 na 40. Katika hatua nyingine Masoud alisema mitambo ya kuchakata gesi imekamilika kwa asilimia 96.
Alisema kukamilika kwa mitambo hiyo inamanufaa makubwa ikiwemo umeme wa uhakika na gharama nafuu kwani utekelezaji wa mradi huo utaliwezesha taifa kuokoa trilioni 1.6 kwa mwaka zinazotumika kununua mafuta kwa ajili yua kuzalisha umeme.
Masoud alisema kukamilika kwa mradi huu kutachochea maendeleo ya viwanda nchini kwani viwanda vingi vimeonyesha nia ya kutumia nishati ya gesi asilimia katika kuendesha mitambo yake ya uzalishaji.aidha umeme wa uhakika utapunguza gharama za uzalishaji na kufanya bidhaa za tanzania kukuzika katika masoko mbalimbali duniani.
Alisema tatizo la ajira nalo litapungua kutokana na kukamilika kwa mradi huu ambao utapelekea ajira mpya nyingi kupatikana na kutokana na kuwepo kwa umeme wa kutosha na uhakika katika viwanda ambapo viwanda vingi vitaanzishwa vilevile umeme utakwenda mashambani na kwenye biashara nyingine hivyo kwa namna moja ama nyingine ajira zitaongezeka.
Alisema gesi hiyo asilia pia hutumika kama malighafi katika viwanda mbalimbali kama,mbolea, kemikali,aluminiamu pamoja na kutengeneza vifaa vya plastiki uanzishaji wa viwanda vipya kutokana na matumizi ya gesi asilimia kutachochea
kukua kwa uchumi wa nchi yetu na kwa upatikanaji wa ajira mpya nyingi kwa vijana wetu. Aliongeza kuwa Serikali kupitia wizara hiyo chini ya Mradi Endelevu wa Usimamizi wa Rasilimali Madini (SMMRP), inakaribisha maombi ya Ruzuku Awamu ya pili kwa wachimbaji wadogo nchini.