Nimapumziko ya Kiapo cha Rais…!

IMG_0752
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.

Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Dk. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.