Mgombea wa ubunge Jimbo la Mtama na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye akizungumza na wapiga kura wake katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
|
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa wamefurika katika viwanja vya Nyangao Jimboni Mtama katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza. |
|
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Mtama leo. |
Na Joachim Mushi, Lindi/Mtwara
MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu leo amemalizia ziara yake ya kampeni za uchaguzi kuinadi ilani ya chama hicho katika majimbo anuai ya Mkoa wa Lindi na kuendelea na ziara hiyo katika Mkoa wa Mtwara huku akiahidi kushughulikia kero za wakulima wa korosho hasa suala zima la ‘Stakabadhi Ghalani’ ambalo wakulima wamekuwa wakilipinga.
Akizungumza katika mikutano yake ya kampeni aliyoifanya katika Majimbo ya Ruangwa, Mtama yaliyopo Mkoa wa Lindi na Jimbo la Ndanda la Mkoani Mtwara; Bi. Suluhu kwa kuanzia serikali itakayoundwa na CCM haitokubali utaratibu wa kuwakopa wakulima wa korosho na imedhamiria kuboresha soko la zao hilo ili kukuza kipato cha mkulima.
|
Kampeni zikiendelea katika mkutano huo Jimboni Mtama leo. |
|
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Nyangao Jimbo la Mtama katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM. |
Akiwa katika Jimbo la Mtama alisema Serikali imepanga kuvichukua na kuvifufua viwanda vyote ambavyo vilichukuliwa na baadhi ya wawekezaji na kuvibadili matumizi jambo ambalo limesababisha zao la korosho kuendelea kufanya vibaya sokoni huku wakulima wakilalama. “…Tutavirejesha viwanda vyote vya korosho vilivyochukuliwa na wawekezaji na kubadilishwa matumizio, tunataka viwanda hivi vifufuliwe na kuendelea na kazi ili kukuza thamani ya mazao ya wakulima,” alisema Bi. Suluhu.
Bi. Suluhu pia alisema kabla ya kuingia madarakani Serikali tayari imeanza kulifanyia kazi suala zima la kero kwa wakulima wa korosho na kwa sasa imetoa bei elekezi ya zao hili ili kuepusha ukandamizaji ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya waranguzi. Alisema bei iliyotolewa kwa sasa ni shilingi 1200 kwa kilo daraja la kwanza na shilingi 960 kwa kilo kwa korosho ya daraja la pili.
Awali akizungumza katika mkutano wa hadhara mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama, Nape Mosses Nnauye alisema endapo atafanikiwa kutwaa ubunge katika jimbo hilo atahakikisha anavipatia umeme vijiji vyote vilivyopo katika jimbo hilo kwa kushirikiana na Serikali ya CCM endapo itaingia madarakani.
|
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Chadema Taifa, Greison Nyakarungu ambaye kwa sasa amejiunga na CCM akielezea madhaifu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo katika moja ya mikutano ya kampeni za mgombea mwenza wa CCM. |
Alisema ndani ya kipindi cha miaka mitano atajitahidi kuhakikisha sehemu kubwa la vijiji vya jimbo hilo vinapata maji safi na salama pamoja na huduma za mtandao wa simu jambo ambalo limekuwa kero baadhi ya maeneo. Pamoja na hayo ameiomba Serikali ya chama chake endapo itafanikiwa kuunda dola kuhakikisha inabadili mfumo wa upelekaji fedha za ruzuku za maendeleo kutoka utaratibu wa kuangalia idadi ya watu hadi pia kuangalia kiwango cha umasikini kwa jamii ya maeneo husika.
Amesema eneo kama la Jimbo la Mtama hali ya kipato cha wananchi ni mbaya licha ya eneo hilo kuwa na idadi ndogo ya watu ukitofautisha na maeneo mengine hivyo kuendelea kupokea kiasi kidogo cha fedha za ruzuku ya maendeleo. Hata hivyo mbunge huyo ameomba Serikali iangalie uwezekano wa kuipa hadhi ya Wilaya Jimbo la Ndanda kwani wananchi wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma.
Akiwa katika Jimbo la Ruangwa mbali na ahadi za uboreshaji wa soko kwa wakulima wa korosho, uboreshaji wa elimu na huduma za afya na huduma zingine muhimu za jamii, Bi. Suluhu alisema ameipokea kero ya barabara za mji huo na Serikali itazifanyia kazi kulingana na utekelezaji wa ilani ya CCM.
|
Baadhi ya wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Ruangwa wakiwa katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM leo. |
|
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ruangwa kupitia CCM, Majaliwa Kasimu Majaliwa akizungumza katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu. |
|
Baadhi ya wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Ruangwa wakiwa katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM leo. |
|
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa wamefurika katika viwanja vya Nyangao Jimboni Mtama katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza. |
|
Ujumbe wa wapiga kura katika mabango anuai kwenye mkutano wa kampeni Jimbo la Mtama. |
|
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa wamefurika katika viwanja vya Nyangao Jimboni Mtama katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza. |
|
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za Urais CCM Taifa, Anjela Kiziga (kushoto) akizungumza katika mkutano wa kampeni. |
|
Mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akizungumza jambo na mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama na Katibu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. |
|
Mgombea wa ubunge Jimbo la Mtama na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye akizungumza na wapiga kura wake katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu. |
|
Msanii Snura Majanga akiburudisha wanaCCM na wapenzi wa chama hicho leo Jimbo la Mtama. |
|
Msanii wa bongo movie, Wema Sepetu akizungumza na umati katika mkutano. |
|
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi. |
|
WanaCCM na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu. |
|
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu. |
|
Viongozi wa dini ya kiislamu wakisoma duwa kabla ya kuanza mkutano wa kampeni katika Jimbo la Ruwangwa. |
|
|