Ngumi Kupigwa Bagamoyo…!

Ngumi Kupigwa Bagamoyo...!
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo na Adam Ngange wa Chanika jijini Dar es Salaam wanatarajia kupanda uringoni Siku ya Jumamosi katika ukumbi wa che kwa che uliopo mjini Bagamoyo. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na waandaaji wa mpambano huo mabondia hao watapima uzito Ijumaa Stendi Kuu ya mabasi Bagamoyo.

Ambapo mabondia hao watamalizia ubishi wao wa nani zaidi kati ya Bagamoyo na Chanika. Taarifa inasema mpambano huo utasimamiwa na Chama cha Ngumi za Kulipwa (P.S.T), na litakuwa na raundi sita na kg 61. Pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi siku hiyo. Rashidi Haruna atakumbana na Kaminja Ramadhani na Harid Hongo atakabiliana na Kishoki Mbishi mpambano mwingine ni Abdallah Samata atakaye zidunda na Maono Alli.

Mpambano hiyo inaletwa kwenu na Sharif Promotion wakati mgeni rasmi siku hiyo ni bondia kutoka morogoro Cosmas Cheka ambaye atakuja kuwapa nasaa mbalimbali mabondia na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuweza kusonga mbele kwa mchezo uho mjini Bagamoyo kingilia katika mpambano uho ni Tsh, 8000 kwa V.I.P na kwaida ni sh. 5000.