Ngoma Africa band watunukiwa , ” IDA – International Diaspora Award”

HABARI za uhakika kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi
barani ulaya “The Ngoma Africa Band” au maarufu kwa jina la “FFU”
wazee wa virungu na makombora ya muziki,yenye makao yake
nchini Ujerumani, Bendi imetajwa kuwa ni bendi bora inayoitangaza miziki
ya Afrika kwa kasi duniani,na imechaguliwa kupewa tuzo maalumu la
” IDA – International Diaspora Award” award , hiyo inatolewa na
tahasisi za kimataifa,itakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo Kamanda
Ras Makunja wa FFU mwanzoni mwa mwezi wa nane.
Inasemekana Sherehe za kukabidhiwa TUZO hiyo zitafanyika mjini Tubingen,
mkoa wa Baden württemberg, kusini mwa ujerumani.
Tahasisi za kimataifa zinazoshughulika na utamaduni wa kimataifa kuanzia
mwaka jana zilianza mkakati kutafuta bendi ya kiafrika inayolitangaza bara
la Afrika kwa kutumia muziki, na kuweka utaratibu wa kuzipigia kura bendi
hizo katika tovuti mbali mbali online na offline,Ngoma Africa Band ikajichulia
ushindi wa mamlioni ya kura, pia imegundulia kuwa bendi hiyi inakubalika na
mamilioni ya washabiki wa mataifa mbali mbali,
Mzimu huo wa muziki kutoka Bongo unadaiwa kuwa na wafuasi milioni
50 duniani kote,hali hii inatishia maporomota wa muziki wa kimataifa,
kuwa FFU ni mali ya mamilioni ya washabiki,ni bendi ambayo kipenzi
cha mamilioni ya washabiki