Ngoma Africa Band kuvamia Munchen Dec 3, 2011

Kundi la wasanii Watanzania kutoka Bendi ya Ngoma Africa iliyopo nchini Ujerumani.

CD ya “50 Uhuru Anniversary” inatamba redioni
Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA waishio Ujerumani wameanza shamra shamra za kusherekea Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kwa kasi kubwa inayotingisha kila kona jijini hapa.

Sherehe hizo zinatarajia kuanzia Mjini München Desemba 3, 2011 ambapo kutakuwa na maonesho mbalimbali ya bidhaa za Tanzania, mavazi na mdahalo rasmi huku usiku kukiwa na burudani ya muziki wa Ngoma Africa Band katika Mtaa wa Siebold Str, 11 ulipo ukumbi husika.

Kuanzia Desemba 9 hadi 10, 2011 mjini Berlin ambako ndipo ulipo Ubalozi wa Tanzania na Mji Mkuu wa Ujerumani, kutakuwa hapatoshi kwani sherehe hizo zitaambatana na uzinduzi wa Jumuia ya Umoja wa Watanzania nchini Ujerumani (UTU). UTU ndio umoja pekee unaowaunganisha Watanzania wote waishio Ujerumani.

Umoja huo uliotiliwa nguvu na balozi Ngemera, umeshasajiliwa na viongozi wake ni Mfundo Peter Mfundo (Mwenyekiti) na Tullalumba Mloge (Katibu), utaratibu unaonesha kuwa sherehe hizo kwa Mji wa Berlin zitaanza majira ya saa 9 mchana hadi majogoo, ambapo Ngoma Africa Band aka FFU, watatumbuiza na muziki wao. Sherehe itafanyika Apostelkirche 1, 10738 Berlin. UMOJA NI NGUVU WATANZANIA JITOKEZENI! KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU! sikiliza muziki at www.ngoma-africa.com