Ngoma Africa Band kuvamia maonesho International African Festival

Baadhi ya wasanii wa kikosi cha Ngoma Africa Band

*Kupokea tuzo ya bendi bora ya kiafrika barani Ulaya

Na Mwandishi Wetu

NGOMA Africa Band a.k.a ‘FFU’ yenye makao yake nchini Ujerumani,
na bendi maarufu barani Ulaya inatarajia kutingisha tena jukwaa la onesho la kimataifa la International African Festival, mjini Tubingen, Ujerumani.

Onesho la kwanza litafanyika Jumamosi ya Agosti 11 na la pili likipigwa Jumapili ya Agosti 12 katika Uwanja wa FestPlatz, Tubingen. Habari za uhakika zinaeleza kuwa bendi hiyo pia imechaguliwa kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya na kushinda tuzo ya ‘IDA – International Diaspora Award”. Tuzo hiyo itakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki mahiri na Kamanda, Ras Makunja siku hiyo.

Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kimepigiwa kura nyingi na washabiki, pamoja na taasisi mbalimbali kwa kutajwa kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika barani Ulaya iliyoweza kutumia muziki
wake kama daraja na kufanikiwa kuziteka nyoyo za washabiki huku ziki waunganisha kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Pia kikosi kazi hiko kimetajwa mara nyingi kuwa kimediliki kujitoa muanga kwa kupiga muziki mpaka kwenye nchi zenye usalama mdogo na mazingira ya kivita! Kwa ujasiri huu Ngoma Africa Band inavuna ilichopanda.

Ngoma Africa band imetajwa kuwa muziki wake umefanikiwa kuzoa mamilioni ya washabiki na kuchangia kwa kiasi kikubwa kutukomeza fikira za kiubaguzi wa rangi zilizomo kwa baadhi ya wazungu barani ulaya.

Ngoma Africa band inasemekana kuwa na washabiki au wafuasi milioni 50 dunia nzima, na washabiki wengine milioni 11 wanapitia tovuti ya bendi hiyo at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com. Usikose kuwasikiliza FFU kupitia; www.ngoma-africa.com