NEC Yamkabidhi Dk Magufuli Hati ya Kuteuliwa Urais

Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kushoto) pamoja na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) wakionesha hati ya uteuzi walizokabidhiwa na Tumea ya Taifa ya Uchaguzi kwa wanaCCM na wananchi waliofika kumlaki katika ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam leo .

Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kushoto) pamoja na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) wakionesha hati ya uteuzi walizokabidhiwa na Tumea ya Taifa ya Uchaguzi kwa wanaCCM na wananchi waliofika kumlaki katika ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam leo .


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imewakabidhi rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Makamu wa Rais mteule, Mama Samia Suluhu Hassan hati za uteuzi kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.

Hafla ya kukabidhiwa hati hizo umefanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, mabalozi, waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa ndani na nje, viongozi wa dini, wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na baadhi ya wagombea nafasi ya urais kutoka vyama vya upinzani, isipokuwa mgombea wa CHADEMA, Edward Lowassa na aliyekuwa mgombea wa CHAUMMA, Hashim Rungwe Spunda ambao hawakuonekana licha ya kuandaliwa viti katika hafla hiyo maalum.

Dk. John Pombe Magufuli ambaye aligombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM alionekana kushangiliwa pamoja na mgombea mwenza, Mama Suluhu mara baada ya kuingia ukumbini huku wananchi hasa wafuasi wa CCM wakisikika wakiimba neno, ‘Rais..rais..rais..rais’. Mara baada ya kukabidhiwa hati hiyo Dk Magufuli aliizungusha kuwaonesha viongozi mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo pamoja na wananchi walioshiriki.

Akizungumza mara baada ya mapokezi katika ofisi ndogo za CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam, alisema malumbano ya uchaguzi yamekwisha hivyo kila mmoja aanze kuchapa kazi kulijenga taifa. Aliwataka Watanzania wote kumpa ushirikiano ili aweze kutekeleza ahadi na matumaini ya wananchi haraka iwezekanavyo.

Amewapongeza Watanzania kwa kuweza kufanya uchaguzi wao kwa amani na utulivu na kuiwezesha nchi kushinda katika uchaguzi na vyombo vya dola kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo, viongozi wa dini kwa maombi ya kuliombea taifa na Rais Kikwete kwa kutoa ushirikiano wa kutosha hadi taifa linafikia hatua ya leo.

“…Nampongeza Rais Kikwete sana kwa ushirikiano na upendo alionao, maana wapo viongozi wengine wa Afrika kila wakikaribia kustaafu wanabadilisha katiba ili waendelee kuongoza lakini kwake haijatokea hivyo…nampongeza sana kwa hilo,” alisema Dk. Magufuli.

Alisema kuwa ili kuonesha dhamira na ari ya kuwatumikia Watanzania kama ilivyokuwa kwa kauli mbiu yake “Hapa Kazi Tu” ataanza kufanya kazi siku hiyo hiyo baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “…Siku hiyo hiyo baada ya kuapishwa nitaingia ofisini na kuanza Kazi…,” alisema Dk. Magufuli.

Baadhi ya wanaCCM na wananchi wengine walioshiriki hafla ya kukabidhiwa hati za uteuzi kwa Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli pamoja na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan leo  jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali waandamizi wa taifa wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa hati za uteuzi kwa Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli pamoja na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan leo  jijini Dar es Salaam.
Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) pamoja na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan (nyuma yake) leo  jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa hati.
Meza kuu katika hafla hiyo Diamond Jubilee Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwakilisha mataifa yao, mabalozi na waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wakiwa katika hafla hiyo.
Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia) akimkabidhi hati ya uteuzi Rais wa Tanzania anayesubiri kuapishwa, Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) kwenye hafla maalum iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubelee Dar es Salaam leo.
Kushoto ni makamu wa Rais anayesubiri kuapishwa, Mama Samia Suluhu Hassan akionesha hati ya uteuzi wa nafasi hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Jaji Damian Lubuva leo jijini Dar es Salaam.
Dk. Magufuli akimuonesha hati ya uteuzi Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, wa kwanza kulia ni Makamu wake Mama Suluhu.
Viongozi mbalimbali wakiwakilisha mataifa yao, mabalozi na waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wakiwa katika hafla hiyo.
Wananchi na wanaCCM wakishangilia jambo katika hafla hiyo.
Dk. Magufuli akipunga mkono juu ya gari akitokea Ukumbi wa Diamond Jubilee kupokea kiapo cha uteuzi.
Dk Jakaya Kikwete akizungumza katika hafla hiyo.
Dk. Magufuli akizungumza ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokewa.
Dk. Magufuli akizungumza ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokewa.
Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli akionesha hati ya uteuzi walizokabidhiwa na Tumea ya Taifa ya Uchaguzi kwa wanaCCM na wananchi waliofika kumlaki katika ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam leo