Ndani ya viwanja vya Saba Saba leo Dar es Salaam

Banda la bunge ndani ya viwanja vya sabasaba, katika maonesho ya 35 yalioanza leo.

Hapa sio shambani, bali ni sehemu ya banda la maonesho la Jeshi la Magereza ndani ya viwanja vya sabasaba. Hizi ni mboga pamoja na mahindi vilivyooteshwa kiustadi.

Hili ni banda la Benki ya NMB ndani ya viwanja vya Sabasaba.

Huduma za kibenki za CRDB ndania ya viwanja vya sabasaba.

Mkurugenzi wa TINY ENTERPRISES, Evelyne Mushi akielezea moja ya bidhaa zinazotengenezwa kwa mmea aina ya Roselle ambao unatumiwa na asasi yake kutengeneza bidhaa mbalimbali jana ndani ya viwanja vya sabasaba. Benk ya NMB imewadhamini asasi mbalimbali na wafanyabiashara kushiriki katika banda hilo.