
Mmoja wa wananchi (kushoto) waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonesho ya 37 ya Biashara, Sabasaba akipata maelezo

Baadhi ya wananchi (kulia) wakipewa maelezo juu ya Siwa ya Bunge la Tanzania toka kwa mmoja wa wafanyakazi wa ofisi ya bunge jana katika Maonesho ya 37 ya Biashara, Sabasaba

Mfano wa kiti cha spika wa Bunge la Tanzania kikiwa katika Maonesho ya 37 ya Biashara, Sabasaba ndani ya banda la bunge.

Baadhi ya wananchi waliotembelea banda hilo wakipewa maelezo ya maspika anuai waliowahi liongoza bunge la Tanzania.

Mhariri Mkuu wa dev.kisakuzi.com, Joachim Mushi akipiga picha ya ukumbusho katika kiti cha Spika ndani ya banda la Bunge la Tanzania alipotembelea banda hilo jana.

Ndani ya Banda la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maonesho ya 37 ya Biashara, Sabasaba
TTCL na Simu za Shilingi 5,000…!

Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakipewa maelezo juu ya simu za mkononi zinazouzwa kwa shilingi 5,000 na 10,000 katika banda hilo jana. Mteja anayenunua simu ya shilingi 5,000 hupewa na muda wa maongezi wa shilingi 5,000 tena.