Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichua taarifa hiyo.
|
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi uliopita. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Sensa za watu na takwimu wa Ofis ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha March 2017 imekuwa sawa na kasi ya upandaji ilivyokuwa mwaka ulioisha.
Kwesigabo, alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.4 mwezi April 2017 kutoka 1o2 mwezi April 2016.
“Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi marchi 2017 kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Aprili imekuwa sawa na mwezi Marchi 2017,”alisema
Pia alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi 11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa mwezi Marchi.
Aidha mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi asilimia 12.0 kutoka asilimia 11.7 mwezi Marchi 2017.
Alisema badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa sisizo za vyakula umepungua kidogo hadi asilimia 3.4 mwezi Aprili kutoka asilimia 3.6 mwezi Ma
chi.
Akizungumzia kuhusu ukuaji wa dhamani ya shilingi, Kwesigabo alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 91 na senti 71, mwezi Aprili 2017 ikilinganisha na shilingi 92 na senti 21 ilivyokuwa mwezi Marchi 2017.