NI mategemeo yetu watanzania wengi kuwa vigogo waliohusika kwa namna moja au nyingine katika sakata la fedha za Tageta Escrow kuwa wanajiuzulu nafasi zao na mkondo wa sheria uwashughulikie haraka kwani hakuna aliye juu ya sheria watanzania wote tupo chini ya sheria.
Vigogo hawa wazito wanahusika kupokea mgao wa fedha za wavuja jasho wa nchi hii lazima washughulikiwe na vyombo vya dola ili wawe mfano kwa wengine kuwa mvunja sheria lazima mkondo wa sheria umshughulikie.
Kwa kila kitu kiko wazi katika sakata zima Tageta Escrow na wahusika wametajwa basi hakuna haja ya kesho keshokutwa,wao wenyewe watuhumiwa wangeachia ngazi kwa kujiuzulu ili kuonyesha uzalendo wao kuwa wanaziheshimu sheria za nchi na katiba. Lingekuwa jambo la kiungwana sana kama wangejiuzulu wenyewe kabla ya kutenguliwa na mamlaka iliyowateua
Baadhi ya vigogo hawa wapo maprofesa, sasa hawa viongozi wetu maprofesa ndio ingekuwa wa mwanzo kuonyesha mfano wa kujiuzulu. Mfano Waziri wa ardhi Prof. Anna Tibaijuka yeye kakubali kwa namna moja kuwa kapokea mgao Tsh. Bilioni 1.6 akidai kuwa ni za shule zake, wakati shule zenyewe kuna baadhi ya walimu kutoka nje ya nchi mabo wanalipwa mishaara kwa dola.!
Ni vema waziri Anna Tibaijuka akaonyesha mfano kwanza wa kujiuzulu. Hili wananchi tujue kuwa sheria ya nchi hii ni msumeno. Pia tungeshauri hati zao za kusafiria au pasipoti za vigogo hawa ziwechukuliwe na idara husika za usalama hadi pale itakapothibitika kuwa hawana hatia.
SHERA MSUMENO UKATE PANDE ZOTE