Nassibu Ramadhani Kuzichapa na Fransic Miyayusho Kugombea Ubingwa wa WBF

Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF. Picha zote na Super d bolog.

Mwandaji wa mpambano wa ubingwa wa WBF, Mohamed Bawazir (katikati) akiwa ameshika mkanda na mabondia Nassibu Ramadhani (kushoto) na Fransic Miyayusho (kulia). Wengine kulia ni Rais wa PST, Emanuel Mlundwa ambao na wasimamizi wa mpambano huo, kushoto ni Mratibu, Paul Kunanga na Kocha wa Nasibu Christopher Mzazi.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI YA Darworld Links imeandaa mpambano mwingine wa ubingwa wa masumbwi utakaowakutanisha bondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho, mpambano utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba. Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mohamed Bawazir alisema wameamua kuwakutanisha mabondia hao baada ya kuona kila mmoja anamtambia bondia mwenzake.

Alisema mpambano huo utamaliza ubishi na kujua nani zaidi ya mwenzake kwa kuwa viwango vyao vina fanana na vinatambulika kimataifa. Amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono hususani kiudhamini kwa mchezo huo wa masumbwi.

Aliongeza kuwa udhamini upo wazi hata kwa bondia mmoja mmoja ili kuwaongezea changamoto mabondia hawa ambao ni vijana huku wakiwa na uwezo mkubwa wa kutangaza biashara mbalimbali kupitia mchezo wao wa masumbwi.

“Makampuni mengi yamekuwa yakiupiga danadana mchezo huu ni mchezo kama michezo mingine nashangaa sana kuona tunakosa. Udhamini tunapoomba sehemu ya makampuni mbalimbali ukienda wanasema hatuhusiki na mchezo huo. Wengine wanajitamba kabisa wadhamini wa michezo wakati wanabagua michezo mingine kama ngumi,” alisema.

Hata hivyo amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza kwa wingi Desemba 9, 2012 kushuhudia mpambano huo wa ngumi ili mchezo huo usonge mbele. Aliongeza kuwa watakaosindikiza mpambano huo wa masumbwi ni pamoja na Fadhili Majia VS Juma Fundi
Moh’d Rashid Matumla VS Doi Miyayusho, Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ VS Said Mundi wa Tanga, Fred Sayuni VS Deo Samweli, Hassani Kidebe VS Baina Mazola.

Mapambano yote ya utangulizi ni mazuri na vijana wanaotakiwa kuendelezwa katika elimu ya masumbwi Duniani ili wawe mabondia wazuri Mpambano huo umedhaminiwa na JB BELMONT HOTEL gazeti la Jmbo Leo, Times FM. Wanaoitaji kudhamini mawasiliano ni kupitia namba 0716 332933, 0784 426542