Nani Mtani Jembe; Simba, Yanga Wavuna Mil 422/-

Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo.

Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo.


MECHI ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)-
mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.
 
Kaimu Katibu Mkuu huyo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, aliongeza asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.
 
Alisema mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.