Nani kucheza fainali kati ya Ilala na Mwanza?

Nembo ya Kili Taifa Cup

Na Asha Kigundula
Arusha

TIMU ya soka ya Mkoa wa Ilala leo itakuwa na kibarua kigumu itakapovaana na timu ya soka ya Mkoa wa Mwanza katika hatua ya Nusu fainali ya michuno ya Kili Taifa Cup inayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani hapa.

Kindumbwendumbwe hicho kitaanza saa 10.00 Alasiri ambapo mshindi wa mchezo huo atamsumbili mshindi wa michezo wa kesho wa hatua hiyo kwa ajili ya kucheza fainali siku ya Jumamosi.

Endapo dakika 90 za mchezo zitamalizika bila ya kupatikana mshindi timu hizo zitapiga penati tano tano ambazo zitatoa mshindi na atakayetolewa atacheza hatua ya kumtafuta mshindi wa tatu siku ya Ijumaa.

Mchezo wa leo unaatabiliwa kuwa mkali na wanguvu kutokana na timu hizo kuwa na uwezo mkubwa katika kusakata kabumbu. Ilala yenye wachezaji waliowahi kuwika katika Ligi kuu kama vile Salum Mpakala, Adam Kingwande Omar Matuta na Anthony Matangalu, katika misumi kadhaa wanaweza wakawanaweza wakawa mwiba mkali kwa timu ya Mwanza iliyona mchezaji wa Yanga Jerry Tegete.

Wadhamini wa Mashindano haya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kwa bia yake ya Kilimanjaro wamekuwa wakimzawadia mchezaji bora wa mechi Sh. 100,000. Bingwa wa Michuano hiyo atanyakuwa kitita cha Sh.milioni 40, mshindi wa pili Sh. milioni 20 wakati wa tatu sh. milioni 10.