Wakati mwingine unaweza kuikinga ajali isitokee na hata kama ikitokea madhara yake yakawa si makubwa, lakini kwa staili kama hii unaweza kujisababishia ajali mwenyewe bila kinga. Mkazi wa Morogoro eneo la Mikumi akiwa amepanda juu ya magunia ya mkaa kwenye pikipiki ya miguu mitatu jambo ambalo ni hatari kwake kama alivyokutwa na mpiga picha wa dev.kisakuzi.com hivi karibuni.