Namna ya Kuanza Siku Yako Vyema

1) Amka kitandani mapema, kama unakuwia vigumu, “set an alarm clock” na uiweke sehemu ambayo huifikii ili uweze kuamka na kwenda kuizima. Vile vile unaweza rafiki yako akupigie simu, kitendo cha wewe kuongea na simu kitakuondolea usingizi bila wewe kujijua na kujikuta umeshaamka.

2) Isalimu siku yako, fungua mapazia na acha mwanga wa jua uingie ndani. Mshukuru Mungu wako kwa kukupa afya njema. Watu wengine wapo “busy” sana wanajisahau kufanya mambo madogo madogo, Ukweli ni kwamba mambo haya hayachukui muda na ni yanafaida kubwa kwako.

3) Kuwa “optimistic” kuhusu siku yako. Unaweza kufanya hivyo kwa kuiangalia kwenye kioo na kusema vitu vizuri vitano kuhusu wewe, vitu kama ” I am the best” au “Nina macho mazuri”. Mambo kama haya yataifanya siku yako kuwa nzuri, hata kama unajiona kama kichaa wakati unafanya hivyo.

4) Jiandae kwa siku yako, neda kaoge, kula chakula cha asubuhi, vaa na jiandae kama ni kwenda kazini au shuleni. Usiruhusu woga au matatizo ya jana yake kukuharibia siku yako.

5) Fikiria kuhusu siku yako na mambo ambayo unataka kuyafanya kwa siku hiyo, andika mahali. Ukiandika vitu ambavyo unataka kufanya, itakusaidia kuona ni namna gani siku yako imekuwa yenye mafanikio.

6) Jiamini kuwa utaweze kutatua tatizo lolote ambalo litatokea kwa siku hiyo.

7) kumbuka usemi huu ” If the life doesnt smile at you, tickle life until it laughs”

8)Imba wimbo wowote ambao una “positive” message.

9) Kula “breakfast” Hii ndio njia bora ya kuanza siku yako na itakusaidia katika siku nzima, ni vyema kula “breakfast” ndani ya lisaa moja baada ya kuamka.

10 Fanya mazoezi. Kufanya mazoezi kunasaidia kutoa “chemicals” kwenye ubongo ambazo zinasaidia kujisikia vizuri.

11) Tabasamu. Ukitabasamu,sio tu inamfanya mtu mwingine ajisikie vizuri, wewe mwenyewe pia uanajisikia vizuri na kukuchangamsha.