Namibia yaingia michuano ya Chalenji

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodger Tenga (katikati) akizungmza na wanahabari leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah (kulia). (Picha na Joachim Mushi)

Na Mwandishi Wetu

NAMIBIA itashiriki michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza Novemba 25 mwaka huu ikiwa timu mwalikwa baada ya Eritrea kujitoa. Akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam leo Rais wa Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodger Tenga amesema Namibia inaingia moja kwa moja katika kundi A ambalo lina mabingwa watetezi Tanzania Bara, Rwanda na Djibouti.

Amesema kuingia kwa timu hiyo kutaleta changamoto kwa timu nyingine ambazo zilizoea kukutana zenyewe mara kadhaa katika mashindano hayo kipindi cha nyuma. Hata Hivyo Tenga amesema mashindano yote yatafanyika jijini Dar es Salaam kutokana na kile kukosa wadhamini katika mikoa mingine ambayo ilipangwa kufanyika huko.

Akitoa ratiba ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia ya Tusker, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah amesema mechi zote zitachezwa Dar es Salaam baada ya Mkoa wa Mwanza kushindwa kutimiza masharti iliyopewa ili nayo iwe kituo cha michuano hiyo.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodger Tenga (katikati) akizungmza na wanahabari leo.


Osiah amesema mechi mbili zitakuwa zikichezwa kwa siku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam isipokuwa Novemba 26 mwaka huu ambapo kutafanyika uzinduzi rasmi saa 10 jioni kwa mechi kati ya Tanzania Bara na Rwanda.

Katibu huyo ameongeza kuwa Novemba 25 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Burundi na Somalia (saa 8 mchana) na Uganda na Zanzibar itakayoanza saa 10 jioni. Akitaja makundi hayo Katibu huyo alisema GROUP A; litakuwa na TANZANIA, RWANDA, NAMIBIA, DJIBOUTI huku GROUP B; likiwa na timu za UGANDA, BURUNDI, ZANZIBAR, SOMALIA. Osiah ameongeza kuwa
GROUP C; litakuwa na SUDAN, MALAWI, KENYA, ETHIOPIA.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodger Tenga (katikati) akizungmza na wanahabari leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah (kulia). (Picha na Joachim Mushi)


Nao wadhamini wa mashindano hayo Serengeti Breweries Ltd (SBL), kupitia kwa Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru wameendelea kuwahamasisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu kuwa wazalendo kwa kudhamini michezo ili nchi iweze kufanya vizuri.

SBL ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo ambayo yamekuwa yakipata umaarufu kadri miaka inavyosonga mbele, na mwaka huu wametoa kiasi cha sh. milioni 823 kudhamini mashindano ya Tusker yanayotarajia kuanza Novemba 25, mwaka huu.