Naibu Waziri Kairuki Akizindua Kitabu cha Mambo 101 Kuhusu Polisi

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akizindua kijitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimeandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ubalozi wa Uingereza Nchini na Taasisi ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia haki za binadamu. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento akifuatiwa na Katibu Mtendaji wa Tume Mary Massay.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akiwaonyesha wadau mbalimbali wa haki za binadamu na utawala bura kijitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza mara baada ya kukizindua kitabu hicho leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento akifuatiwa na Katibu Mtendaji wa Tume Mary Massay.

Wadau mbalimbali wa haki za binadamu na utawala bora wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimeandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ubalozi wa Uingereza Nchini na Taasisiya ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia haki za binadamu.