Ofisa Maendeleo ya Jamii Idara ya Kuondoa Umasikini, William Ghupi akimpa maelezo Naibu Waziri, Janet Mbene juu ya huduma anuai zinazotolewa na kitengo hicho kilichopo chini ya Wizara ya Fedha.
Ofisa Masoko Benki ya Posta, Godbright Mlay akimpa maelezo Naibu Waziri Wizara ya Fedha, Janet Mbene juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.
Ofisa Mradi wa Huduma ya Popote Akounti, Catherine Ntangeki akimkabidhi Naibu Waziri, Janet Mbene kadi ya benki ya akaunti ya popote mara baada ya kufungua, katika banda la Wizara ya Fedha.
Ofisa Utumishi wa GPSA, Leah Yeriko akimfisha beji yenye nembo ya taifa Naibu Waziri, Janet Mbene alipotembelea banda hilo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedh, Janet Mbene akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara ya Fedha leo.
Ofisa Mawasiliano Mfuko wa PSPF, Hawa Kikeke (wa kwanza kushoto) akimpa maelezo Naibu Waziri Mbene, juu ya mafao anuai yanayotolewa na mfuko huo.
Naibu Waziri Wizara ya Fedha, Janet Mbene akiwa katika taasisi ya TIA, akipokea maelezo juu ya huduma anuai zinazotolewa na banda hilo, anaezungumza (kwanza kulia) ni Ofisa Mawasiliano wa TIA, Lilian Mpanju
Ofisa Masoko Muandamizi, wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi (GEPF), James Mlowe akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Mbene juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo
Naibu Waziri Wizara ya Fedha, Janet Mbene akiondoka katika banda la wizara ya Fedha mara baada ya kutembelea taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara ya Fedha.